About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Tuesday, January 10, 2012

ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUNYOFOA ROHO YA MWENZIE KWENYE UGOMVI WA POMBE ,TUKIO JINGINE MAMA ALIPUKIWA NA TAA YA KANDILI NA KUSABABISHA KUUNGUA KWA MWILI MZIMA

Na Gideon Mwakanosya,Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linamshikilia Manywele Abdalah Manywele (34)mkazi wa Kijiji cha Chiwana Mashambani kilichopo Kata ya Mbesa Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo Bakari Mohamed(35) mkazi wa kijiji hicho wakati walipokuwa wakigombana kwenye kilabu cha pombe za kienyeji
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo limetokea januari 8 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi huko katika kijiji cha Chiwana Mashambani
Kamuhanda amefafanua kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio watu hao wakiwa kwenye kilabu cha pombe za kienyeji huku wakiwa wanakunywa pombe ghafla ulitokea ugomvi ambao unadaiwa kuwa chanzo chake walikuwa wakigombania pombe na baadae wakiwa wanaendelea kupigana Mohamed alipigwa na kufa papo hapo
Alisema kuwa baada ya kutokea tukio hilo uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho waliotoa taarifa kwenye kituo cha Polisi cha Tunduru na baadae Askari Polisi wakiwa wameongozana na Daktari walifika kwenye eneo la tukio na kumkuta Mohamed akiwa amesha kufa
Ameeleza zaidi kuwa Askari Polisi wakiwa kwenye eneo la tukio walifanya upelelezi wa awali na walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye alikiri kuwa walikuwa na ugomvi kati yake na Mohamed ambaye amefariki dunia
Hata hivyo Kamanda Kamuhanda amesema kuwa Polisi inaendelea kufanya upelelezi zaidi ili kuubaini ukweli wa tukio hilo na kwamba utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakama kujibu shtaka litakalomkabili
MWISHO
TAA YA KANDILI YALIPUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI WILAYANI MBINGA
Na,Gideon Mwakanosya,Songea
MWANAMKE mmoja Theresia Nombo(27) Mkazi wa Kijiji cha Burma wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma amelazwa katika Hospital ya Misheni ya Litembo baada ya kuungua moto mwili mzima wakati alipokuwa anaongeza mafuta kwenye taa yake ambayo baadae taa hiyo ililipuka na kumuunguza mwili mzima
Kamanada wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 4 mwaka huu majira ya saa 3 usiku nyumbani kwake huko katika kijiji cha Burma
Kamanda Kamuhanda amebainisha zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Nombo alikuwa amechukua taa yake na kuiwasha na muda mfupi aligundua kuwa taa hiyo haina mafuta
Alieleza zaidi kuwa Nombo baada ya kugundua taa yake haina mafuta alichukua chupa ambayo alikuwa amehifadhia mafuta ya taa kisha alikwenda hadi ilipotaa yake na kuongeza mafuta kwenye taa yake ya kandili ndipo ghafla kandili hiyo ilianza kulipuka na kupasua chemli na moto kuanza kuwaka na kumsababishia majeraha mwili mzima
Amesema kuwa baada ya kutokea tukio majirani walimchukua Nombo na kumkimbiza katika Hospital ya Litembo kwa ajili ya matibabu ambako amelazwa na hali yake bado ni mbaya sana
MWISHO

No comments:

Post a Comment