Na Gideon Mwakanosya,Songea
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 37 na miezi 6 jela Mtawa(Bruda) Aidan Mhuwa wa Abasia ya Peramiho jela baada ya Mahakama hiyo kumtia hatiani kwa kosa la kuibia Abasia hiyo shilingi milioni 105 na kuamliwa kuresha fedha hizo baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake.
Akisoma hukumu hiyo juzi kwa zaidi ya masaa matatu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Baptisa Mhelela alisema Mahakama hiyo imemtia hatiani Bruda huyo wa Shirika la watawa la Wabenediktine lililo chini ya Kanisa Katoliki jimbo kuu la Songea baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka mahakamani hapo na kwamba itakuwa ni fundisho kwa Watumishi wengine wa Mungu wanye tabia za kuyaibia makanisa.
Hakimu huyo alifafanua kuwa Bruda huyo alitiwa hatiani kwa makosa 14 ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kufungwa kila kosa miaka mitatu na kwamba adhabu hizo zote zinakwenda kwa pamoja hivyo Mshtakiwa atatumikia adhabu ya miaka mitatu jela na kutakiwa kurejesha Shilingi milioni 105 atakapomaliza kutumikia kifungo chake.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa Mahakama hiyo ilizizima kwa huzuni na ndugu wa Mshtakiwa walionekana kuwa na simanzi huku Mshtakiwa akibubujikwa na machozi na mikono yake ikiwa imefungwa pingu akilelekea kwenda kuanza maisha mapya ya gerezani.Mshtakiwa huyo anadaiwa kuliibia Shirika hilo kati ya mwaka 2006 na mwaka 2007.
Katika kesi hiyo ya mwaka 2009 Hakimu Mhelela alisema kuwa katika mashtaka 72 yakiongozwa na shtaka la kuiba vifaa vya ujenzi wa Mradi wa jengo la Abasia ya hanga hiyo Mshtakiwa alishinda lakini alitiwa hatiani kwa kosa la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Alisema kuwa Mshtakiwa huyo alitumia jina bandia la Joseph Nchemeka wakati akisimia Mradi wa jengo hilo na kufungua Akaunti NBC tawi la Ubungo jijini Dar es salaam yenye namba 02221111913 akidai kuwa mtu huyo ni Mkandarasi Mshauri na kwamba hiyo ndiyo akaunti yake wakati mtu huyo ni yeye mwenyewe.
Alisema kuwa ilibainika kuwa mtu huyo ni yeye mwenyewe baada ya kutumwa wakaguzi na kugundua hayupo mtu mwenye jina hilo kwenye orodha ya Wataalamu wa majengo na ndipo Viongozi wa Abasia walipofuatilia na kugundua wizi huo na kwamba ada za ushauri zililipwa kwa jina hilo bandia.
‘Mahakama ilijenga mashaka makubwa kwa nini Bruda Adani atumie jina bandia kufungua Akaunti badala ya jina la Abasia au kwa nini asitumia jina lake ili kundoa mashaka na katika kufuatilia kama hayo ni miongoni mwa majina ikaonekana hayo si majina yake kwa misngi hiyo basi Mahakama imemtia hatiani kwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu’alisema Hakimu huyo wakakati akisoma hukumu hiyo.
Kabla ya ya kutiwa hatiani Bruda huyo alijitetea kuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo na kwamba ana ndugu wanaomtegemea hivyo aliomba mahakama impunguziwe adhabu na ndipo Hakimu Mhelela alieleza kuwa Bruda Aidan katika kosa la kwanza anaukumiwa katika kifungo cha miaka 6 jera, kosa la pili mahakama inampa adhabu ya kifungo cha miezi 12 jera na kosa la 3 hadi la 14 mshtakiwa atatumikia kifungo miaka 3 kila kosa lakini adhabu zote zitakwenda pamoja hivyo atatumikia kifungo kwa muda miaka 3.
MWISHO
No comments:
Post a Comment