About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Tuesday, February 7, 2012

WAKAMATWA KWA KUKUTWA NA MISOKOTO 19 YA BANGI NA WAKIVUTA BANGI NA

                KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMUHANDA

Na Gideon  Mwakanosya, Songea

POLISI  mkoani  Ruvuma imewatia mbaroni wakazi kumi na tatu wa Songea mjini kwa tuhuma za kukutwa wakivuta  bangi na pia wakiwa na misokoto kumi na tisa na glamu 250 ya bangi  ndani ya uwanja wa  michezo wa majimaji wakati wa mashindano ya mpira wa miguu ligi ya daraja la kwanza ngazi ya taifa kati ya timu ya Majimaji na JKT Mlale.

Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda zimesema kuwa tukio hilo lilitokea  February 4 mwaka huu majira saa kumi na moja na nusu jioni ndani ya uwanja wa Majimaji ambapo watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na kiongozi wao Ally Hassani (20) mkazi wa majengo Songea.

Kamhanda alisema kuwa wakati timu za Majimaji na JKT Mlale zikiendelea kucheza kwenye mpambano wa ligi ngazi ya kwanza ya Taifa watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa waliendelea kuvuta bangi na Ally Hassani  ndiye anadaiwa kuwa alikuwa akipita kuiuza.

Alifafanua kuwa watuhumiwa wote kumi na tatu ambao wengine hakuwataja majina, watafikishwa Mahakamani mara tu upelelezi wa tukio hilo utakapo kamilika na kwamba kwa hivi sasa polisi inaendelea kuwasaka wengine ambao wanadaiwa kuwa walikimbia pindi walipoona wenzao wanakamatwa na polisi.

Katika pambano hilo ambalo lilihudhuliwa na wapenzi wa Club za majimaji  na JKT Mlale  katika pambano hilo pamoja na kuwepo purukushani zilizo sababishwa na watuhumiwa hao mpira uliendea kuchezwa hadi dakika ya mwisho ambapo majimaji na JKT Mlale zilitoka bila bila.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment