Na Augustino Chindiye Tunduru
IMEELEZWA kuwa Uchakavu wa Miundombinu ya Majengo ya Mahakama za Mwanzo Wilayani Tunduru Moani Ruvuma na kutokuwepo kwa Watumishi wa Kutosha katika Idara hiyo ni kikwazo kikubwa cha upatikanaji wa haki kwa wakati.
Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazo mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo Geofrey Muhiuni wakati akiongea na wadau wa Sheria katika maadhimisho ya siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Wilaya hiyo.
Akifafanua taarifa hiyo Muhini alisema kuwa Wilaya hiyo inayotambulika kuwa na Mahakama 9 na Mahakama 3 tu ndizo zenye majengo yenye sifa za kufanyiwa hazi na mahakama 6 zilizobakia majengo yake
yapo hoi bini taabani.
Katika Taarifa hiyo Bw. Muhini alibainisha kuwa uchakavu huo mkubwa wa majengo hayo ya kutolea haki unazukabiri Mahakama za mwanzo Nakapanya,Lukumbule,Mtina, Namasakata Matemanga na Nalsi.Alisema kufutia hali hiyo Wananchi wengi wamekuwa wakitembea umbali mrefu ili kufuata huduma hiyo ambayo imekuwa ikipatikana katika Mahakama ya Mwanzo Mlingoti iliyopo Mjini Tunduru hali ambayo
imesababisha kuwepo kwa mlundikano wa kesi.
Akizungumzia upungufu wa ikama ya watumishi katika idara hiyo alisema kuwa kati ya Mahakama hizo Tisa zinazotakiwa kutoa huduma hiyo mbali na uchakavu wa majengo yake idara hiyo inao Mahakimu Watatu tu (3)hali amyo imekuwaa ikiwawia vigumu kutembelea katika mahakama zote ndani katika kipindi cha wiki.
Alisema pamoja na idara hiyo kukabiliwa na upungufu huo mkubwa wa mahakimu pia ina upungufu mkubwa wa watumishi katika ngazi za Ukarani,Walinzi na wahuduma hali mbayo huwafanya mahakimu hao kufanya
pia baadhi ya kazi zilizotakiwa kufanywa na watumishi wa idara hizo.
Awali akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Madaha, Afisa tarafa wa Tarafa ya Mlingoti Manufredi Hyera aliwataka wadau hao kutoa elimu kwa watu wanao waznguka ili watambue umuhimu wa kutii sheria na kwamba kutoifahamu Sheria siyo kisingizio cha kufanya makosa.
Upande wa ujumbe uliotolewa kupitia Wimbo wa Kwaya kutoka katika kikundi cha Uwanja wa Ndege Mjini hapa uliwasomba mahakimu kuangalia uwezekano wa kutoa adhabu Mbadala wakati wanapotekeleza wajibu wao badala ya kila mtuhumiwa kuhukumiwa kutumikia adhabu ya kifungo Gerezani zikiwa ni juhudi za kupunguza mirundikano katika Magereza yote Nchini.
Mwisho
No comments:
Post a Comment