About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, February 3, 2012

WATU SITA MBARONI KWA UPORAJI WA KUTUMIA BARUTI

KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMUHANDA

Na Nathan Mtega,Songea  
 
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu sita wanaodaiwa kuwa ni majambazi ambao walivamia nyumba mbili za wafanyabiashara wa kijiji cha Mkongotema eneo la Madaba Songea vijijini na kufanikiwa kupora zaidi ya shilingi milioni 415600 baada ya kufyatua milipuko mara nne hewani na kusababisha sintofahamu miongoni mwa wananchi wa kijiji hicho.
 
 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesena kuwa tukio hilo lilitokea Januari 31 mwaka huu majira ya 7:30 usiku ambapo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Baraka Bedo(25) mkazi wa Morogoro,Salum Ahmad(45) mkazi wa Mtwara na Stanley Mtega(20) mkazi wa Ludewa mkoani Iringa.
 
Wengine ni Peter Mbilinyi(35) mkazi wa kijiji cha Mkongotema,Mfaume Rashid(30) mkazi wa kijiji cha Hanga ngadinda na James Mtewele(21) mkazi wa kijiji cha Magingo wilayani Songea vijijini.
 
Alifafanua kuwa inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio watu wasiofahamika wakiwa na milipuko na mapanga waliivamia nyumba mbili ikiwemo ya Remigius Ngunja na Egno Mgeni na kufanikiwa kupora fedha taslimu kiasi cha shilini milioni 4.156.000 kabla ya uvamizi huo watuhumiwa hao inadaiwa kuwa walifyatua milipuko minne hewani na kumjeruhi Reimigius  kwa mapanga kichwani na mgongoni.
 
Alisema kuwa baada ya Remigius kupigwa alianguka na kuzirai ndipo mke wake Octaviana Danda walimuamuru atoe fedha huku wakimtishia kumkata mikono kwa kutumia panga walilokuwa nalo ndipo mke huyo alichukua shilingi milioni tatu na kuwakabidhi watu hao pamoja na simu mbili za mkononi.
 
 Kamanda kamuhanda alieleza zaidi kuwa baadae watuhumiwa hao walikwenda kwenye nyumba nyingine ya Egno Mgeni na kumkuta mlinzi wake Avito Mbilinyi na kumuaru awaonyeshe mahali alipo tajiri kisha walifyatua milipuko mitatu hewani na baadae walimkuta mkewe Mgeni na kumuuliza aliko mumewe ambaye alikataa kuonyesha mumewe alipolala na baadae walifanikiwa kumuona ndani ya nyumba na kumuomba awaonyeshe mahali alipo tajiri na mmiliki wa nyumba hiyo.
 
Alibainisha zaidi kuwa mmiliki wa nyumba hiyo hayupo kisha wakaenda kumvamia mkewe na kumuamuru atoe fedha ndipo alipowakabidhi shilingi milioni 1.126.000 na kisha wakatokomea na kwenda kusikojulikana.
 
 Kamuhanda alieleza kuwa polisi walipata taarifa ya tukio hilo kwa njia ya simu na kwenda eneo la tukio na baadae walisimamisha gari lenye namba za usajili T435 BHT Coaster ya abiria inayofanya safari zake kati ya Madaba na Songea mkoani humu ambao walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi watatu ambao ni Edo,Ahmad na Mtega.
 
Ambao walikutwa na kitambaa chenye damu,nguo zilizolowa damu milipuko,betri simu ya mkononi aina ya Nokia,fedha taslimu kiasi cha shilingi 758.000 pamoja na milipuko ambayo ilikuwa imeandaliwa kwa kuweza kulipuka muda wowote.
 
Amesema kuwa watuhumiwa wote wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
 
Mwisho.

No comments:

Post a Comment