About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, February 11, 2012

WAWILI WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KWA KUDHANIWA MAJAMBAZI

WAWILI WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KWA KUDHANIWA MAJAMBAZI
Na Gideon Mwakanosya, Songea
WATU  wawili kati ya wanne ambao majina yao haya kuweza kufahamika wameuawa kwakupigwa na kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali katika eneo la Ruhuwiko Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na kamanda polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda tukio hilo limetokea February 8 Mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi eneo la Ruhuwiko nje kidogo ya mji wa Songea.
Kamanda Kamuhanda alisema kuwa siku hiyo ya tukio inadaiwa watu wanne wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki mbili tofauti walikwenda katika eneo la Ruhuwiko ambako walimkuta mwanamke mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa alikuwa anafunga mbuzi wake kwenye eneo la malisho ambaye walimsalimia na kumuuliza kama anamfahamu msichana mmoja aitwaye Neema.
Alisema kuwa mwanamke huyo badaye aliwajibu kuwa huyo Neema hamfahamu lakini baadaye aliwahoji awaeleze sababu wanayo mtafutia jambo ambalo lilipelekea kuwa na mashaka na watu hao ambao baadaye waliondoka na kuelekea mbele zaidi kwa lengo la kumuulizia msichana huyo ambako walikutana na watu wengine na waliwauliza kama wanamfahamu msichana Neema ambapo watu hao walianza kuwauliza mahali wanapo tokea.
 Alifafanua kuwa watu hao baada ya kuona kuwa majibu yao yana utata ghafla watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walianza kukimbia na kutokomea kusiko julikana na  kuwaacha wenzao wawili jambo ambalo lililowafanya kuwa na mashaka na watu hao kisha walianza kuwapiga huku mmoja kati ya watuhumiwa hawa alifungwa kamba na baadaye waliwachoma moto.
Alieleza zaidi kuwa wakati wananchi hao wanaendelea kuwapiga watuhumiwa walikili kuwa ndio waliohusika katika matukio matatu ya mahuaji yaliyo tokea katika kipindi cha mwezi mmoja ambapo inadaiwa katika eneo la Ruhuwiko kumekuwa na wimbi la wasichana kuuawa na watu wasiofahamika.
Alibainisha zaidi kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja wasichana watatu wameuwawa katika mazingira ya kutatanisha inadaiwa kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo vya kinyama wanatoka nchi jirani ya msumbiji ambao licha ya kuwa uhakika wa jambo hilo bado haujafahamika na polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kufuatia kuwepo uvumi wa watuhumiwa hao ambao wamekuwa wakiwavamia wasichana na kuwauwa kisha wamekuwa wakiwakata baadhi ya sehemu za siri na kwenda nazo nchi jirani ya msumbiji ambako wamekuwa wakichimba madini.
Kamuhanda alieleza kuwa baada ya muda si mrefu polisi walipata taarifa ya tukio hilo na walikwenda eneo la tukio hilo ambako waliwakuta watuhumiwa hao wakiwa tayari wameuawa na wananchi wenye hasira kwa kuchomwa moto ambapo maiti hao walichukuliwa na jeshi hilo na kupelekwa kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Serikali ya Mkoa Songea ambako mamia ya wakazi wa manispaa hiyo walifulika kwa ajiri ya kutambua maiti hizo na kuwafanya polisi waweke ulinzi mkali  katika milango ya kuingilia katika  hospitali hiyo ili kudhibiti usalama wa wagonjwa waliofika kutibiwa na waliolazwa katika hospitali hiyo .
Hata hivyo polisi inamshikilia mwanamke mmoja kwa mahojiano zaidi na kuwataka wananchi kujichukulia sheria mkononi na amedai kuwa polisi inaendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo .
 Mwisho

WAWINDAJI HARAMU WAWILI WAKAMATWA KWENYE HIFADHI YA WANYAMA
Na  Mwandishi Wetu, Songea
WAWINDAJI haramu wawili wakazi wa Kijiji cha Muhuwezi Wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya gobole kwenye mbuga ya hifadhi ya wanyama poli iliyopo kijijini Muhuwezi.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya 12: 30 jioni huko katika mbuga ya wanyama poli ya muhuwesi  eneo la kata ya kalulu wilayani humo.
 Kamuhanda aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Habedi Kahama (25) na Mohamed Mohamed (29) wote wakazi wa kijiji cha Shauritanga kilichopo wilayani Tunduru ambao inadaiwa siku hiyo ya tukio wakiwa katikati eneo la mbuga la wanyama ghafla walijikuta wako mikononi  mwa Askari wa kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Kusini ambao walikuwa wakifanya doria kwenye eneo hilo.
Alfafanua kuwa watuhumiwa hao inadaiwa waliingia kwenye mbuga ya hifadhi ya wanyama bila ya kuwa na kibali na walikutwa wakiwa na silaha ambayo inahofiwa kuwa imekuwa ikitumika na watuhumiwa hao kuwinda wanyama bila ya kuwa na leseni.
 Alieleza zaidi kuwa askali wa kikosi cha kuzua ujangili waliwakamata watuhumiwa hao wakiwa na silaha aina ya gobole isiyo kuwa na namba wala kibali cha kumiliki silaha hiyo na kwamba watuhumiwa ni wahindaji haramu kwenye eneo la mbuga la wanyama la Muhuwesi.
Hata hivyo Kamanda Kamuhanda alisema kuwa kwa sasa hivi taratibu zinafanywa za kuwafikisha watuhumiwa hao Mahakamani mara tu upelelezi utakapo kamilika.
 Mwisho.

No comments:

Post a Comment