About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, February 9, 2012

TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA

Diwani wa Kata ya Mletele, Halmashauri ya Manispaa ya Songea Fravian Tamaambele Legele (Mzee Panya) enzi za uhai wake

Taarifa za kifo cha Mzee Panya zilianza kusambaa majira ya asubuhi leo, baada ya mtandao huu kuwasiliana na ndugu na jamaa wa Marehemu Mzee huyo, walithibitisha kutokea kwa msiba huo

Marehemu Mzee Panya kama alivyokuwa anapenda kujiita mwenyewe, alianza kuugua ghafla mwishoni mwa mwezi wa kwanza akiwa njiani anatoka Wilayani Tunduru ambako alikuwa anafanya shughuli ya kutekeleza mradi wa ujenzi

Ikumbukwe kuwa Mzee Panya licha ya kuwa Diwani mwenye hekima na busara alikuwa ana kampuni yake ya ukandarasi ambayo ilikuwa inatekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma

Mzee Panya alikimbizwa Hospital ya Mkoa wa Songea kwa ajili ya matibabu ambako alilazwa hadi mauti yana mkuta hii leo majira ya asubuhi

Toka uchaguzi mkuu wa Wabunge, Madiwani na Rais ufanyike Octoba 30 mwaka 2010, Mzee Panya ni Diwani wa pili kufariki ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea, kwani wa kwanza alikuwa ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Ally Said Manya ambaye alifariki mwaka jana 2011 katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho

Mtandao huu, utaendelea kuwaletea habari zitakazokuwa zinajiri kwenye eneo la mazishi huko nyumbani kwake Mletele

Bwana alitoa, bwana ametwa jina lake lihimidiwe,
Sote tu wasafiri yeye ametangulia nasi tunamfuata
Roho yake na Roho za marehemu wengine wastarehe kwa amani
                ############# AMINA ##############

No comments:

Post a Comment