About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Sunday, March 18, 2012

NYUMBA 946 ZALIPOTIWA KUBOMOKA WILAYANI TUNDURU

                   Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha

Na Steven Augustino,Tunduru

NYUMBA  946 zimeripotiwa kubomoka kutokana na  mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mfululizo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na kuwaacha wakazi wake wakiwa hawana makazi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru, Afisa Tarafa wa tarafa ya Matemanga  Ally Hatibu na kuongeza kuwa pia mvua hizo zimebomoa vyoo 35 na kusomba mazao katika mashamba ya wakulima 56 na kwama hivi sasa wananchi hao wanahifadhiwa na Ndugu, jamaa na marafiki katika maeneo yao.

Hatibu aliendelea kueleza kuwa pamoja na matukio hayo pia. Mvua hizo zimeharibu vibaya  miundombinu ya barabara, Madaraja  yanayounganisha kati ya Wilaya hiyo na makao makuu ya Mkoa huo barabara za kwenda vijijini.

Akifafanua taarifa hiyo  Hatibu alisema kuwa Tarafa ya Milingoti ndiyo iliyo athirika zaidi kutokana na kubomokewa na nyumba 716 huku takwimu zikionesha kuwa tarafa ya Lukumbule ikifuatia kwa kuwa na nyumba 230 zilizo bomoka kufuatia mvua hizo.

Aidha takwimu za maafa hayo zinaonesha kuwa Kata ya Nakayaya ndiyo inayo ongoza kutokana na kubomokewa na Nyumba 122, Kata ya Milingoti 99, Masonya 88, Nanjoka 57,Mchangani 54 huku kata ya majengo ikishika nafasi ya mwisho kutokana na kubomokewa na nyumba 46.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo daraja lililobomoka ni la mto Masonya liliteteleka kutokana na mto huo kujaa pamoja na madaraja ya mito Nasanga na Msinjewe pamoja na mto Mkandu barabra iendayo katika vijiji vya tarafa za Lukumbule, Nalasi na Mchoteka na kusababisha usumbufu
kwa wanananchi kutokana na baadhi ya magari kusitisha safari za kwenda na kuingia mjini Tunduru huku kukiwa na wimbi la ongezeko la nauli kwa magari yanayokubali kufanya safari hizo kwa kubahatisha.

Hatibu aliendelea kubainisha kuwa miongoni mwa usumbufu unaowapata madereva wanaofanya safari katika maeneo hayo  ni pamoja na kutozwa fedha na wananchi walio panga miti katika maeeenero yaliyo haribika na kuwatoza kati ya Shilingi 5000 na Tsh.2000 kwa kila gali linapo vuka kuelekea upande wa pili.

Alisema kufuatia hali hiyokamati ya Ulinzi na usalama ililazimika kuwatembelea wahanga na kuwapa pole kwa mkasa huo pamoja na kujionea uharibifu wa madaraja hayo na kupeleka taarifa za maafa hayo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ili kuangalia uwezekano wa wahanga hao kupatiwa msaada Serikalini.

Kuhusu uharibifu wa miundombinu ya Barabara na madaraja hayo, Hatibu alisema kuwa tayari Meneja wa Wakara wa Barabara Mkoa wa Ruvuma (TANROAD`s) amekwisha tuma wataalamu Wilayani humo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa barabara zote zinafunguka na shughuli kuendelea kama kawaida.

Mwisho

No comments:

Post a Comment