About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, March 16, 2012

RC ENG, MANYANYA AWATIMUA WAKURUNGENZI WA HALMASHAURI ZA MKOA WA RUKWA KIKAONI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ENG, Stella Manyanya(Mb)
Na Stephano Mango, Rukwa
MKUU wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, aliwafukuza kwenye mkutano wakurugenzi wote wa halmashauri za mkoa huo kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina kuhusu madai ya fedha za walimu.
Manyanya alilazimika kufanya hivyo jana wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) alichokuwa mwenyekiti wake ambapo alipewa taarifa za walimu kutolipwa zaidi ya sh milioni 6.5 wanazoidai Halmashauri ya Sumbawanga Mjini.
Akieleza madai ya walimu hao Ofisa Tawala Msaidizi mkoani hapa David Kilonzo alisema walimu hawajalipwa kwa muda mrefu sasa hususan waliotoka nje ya mkoa huo kwa ushawishi wa mfuko wa kuboresha mazingiara ya watumishi.
Baada ya maelezo ya ofisa tawala huyo, mkuu wa mkoa alichukizwa na kuwatoa nje ya kikao hadi watakapopata majibu sahihi ni jinsi gani watawalipa walimu hao.
Alisema mara ya mwisho niliwaeleza kuwa sihitaji kusikia tena suala hilo likijirudia kwenye kikao cha RCC na niliwaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha mnawalipa walimu lakini hii leo mnakuja na porojo hizo hizo sasa natamka kuwa siwahitaji humu ndani tokeni nyote na mkirejea mniambie namna mtakavyowalipa walimu hao haraka
Alisema serikali inabebeshwa lawama kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya watendaji wake na kwamba inashangaza kuona katika malipo yenu na hata posho zenu mnavyohangaika ili mjilipe haraka lakini madai ya walimu yanachukua muda mrefu huku mkiwazungusha mara nenda mara rudi!
“Mkifanya kazi kwa kufuata taratibu na kuwajibika mtakuwa rafiki zangu lakini kama kuna mtu anapuuza maelekezo yanayotolewa kamwe sitamvumilia na tutamshughulikia kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo.” Alisema Mhandisi Manyanya
Hata hivyo baada ya dakika 45 wakurugenzi hao walirejea kwenye kikao hicho wakidai watahakikisha walimu hao wanalipwa madeni yao katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa.

No comments:

Post a Comment