Na, Stephano Mango, Rukwa
MKUU wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya amewapongeza Madaktari na wauguzi wote nchini ambao walifanya kazi zao kwa umakini mkubwa na uadilifu katika kipindi chote cha mgomo wa kwanza na wa pili ulioitishwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na kumalizika hivi karibuni
Akizungumza jana kwenye kikao cha Kamati ya mkoa wa Rukwa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo alisema kuwa Madaktari na wauguzi wa Rukwa wametujari na kutuheshimu sana
Mhandisi Manyanya alisema kuwa wanataaluma hao wamejari uhai wa watanzania wenzao kwa kudiriki kufanya kazi yao ya kuwatibu wagonjwa na kutoa huduma stahiki za kiafya bila kinyongo wakati wenzao wakiwa kwenye mgomo
Alisema kuwa kitendo chao cha kuwajali wananchi katika kipindi hicho kigumu hivyo , mkoa unajipanga ili kuona namna bora ya kuwapongeza Madaktari na wauguzi wa mkoa wa Rukwa kwa heshima na utu waliouonyesha katika wakati huo na sasa ambapo mgomo nchi nzima umemalizika
Alieleza kuwa wakati wa mgomo maeneo mengine huduma zilisitishwa na kupelekea watu wengi kupata usumbufu, ulemavu wa maisha, vifo na madhara mengine mengi hali ambayo imelitia doa Taifa hili ambalo linajali misingi ya haki za binadamu
"Watanzania tunapaswa tuimarishe maadili ya kazi zetu na kujali utu wa binadamu kwani inasikitika Madaktari na wauguzi wanashindwa kuwahudumia wagonjwa na badala yake wanaendekeza mgomo wenye maslahi binafsi huku wakiwaacha wagonjwa wakifa kwasababu ya kushindwa kumaliza madai yao kwa njia ya kukaa mezani"alisema Mhandisi Manyanya
Alifafanua zaidi kuwa haki ya kuishi ni haki kubwa kuliko zote na kwamba hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuondoa uhai wa mwenzake kwa sababu yoyote ile kwani mwenye uwezo na mamlaka hayo ni mwenyezi mungu peke yake ni vema kazi yake tukamuachia yeye
Aliesema kuwa mkoa wa Rukwa unampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumaliza mgomo huo wa Madaktari nchini na kuahidi kutekeleza baadhi ya madai yao hilo ndilo jambao ambalo watanzania wengi walikuwa wanarisubiri kutokana na kuchoka kwa madhara yaliyokuwa yanajitokeza kutokana na mgomo huo ,hivyo Madaktari wale waliogoma warejee kazini na kuendelea na kazi wakati madai yao yanafanyiwa kazi na Serikali
MWISHO
No comments:
Post a Comment