About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, March 30, 2012

TIMU YA MLALE JKT YAMWAGIWA VIFAA VYA MICHEZO

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu
Na Augustino Chindiye, Songea

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ametoa vifaa vya Michezo kwa timu ya JKT MLALE ambayo ndio timu pekee ya Mkoa huo iliyotinga katika hatua ya Tisa Bora ya Ligi ya Taifa daraja la kwanza.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni Mipira 16, na viatu jozi 25 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 2.5, zikiwa ni juhudi za serikali ya Mkoa huo kukamirisha maandalizi ya timu hiyo itakayowakilisha Mkoa wa Ruvuma katika Ligi hiyo inayo tarajia kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu.

Akiongea katika makabidhiano ya msaada huo Mkuu wa mkoa Mwambungu pamoja na mambo mengine ali toa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kuunganisha nguvu zao na kuiunga mkono timu yao.

Alisema baada ya timu ya Majimaji kufanya vibaya katika ligi hiyo hivi sasa mkoa wake umeelekeza nguvu katika timu hiyo wakiwa na matumaini kuwa timu hiyo ita watoa kwa kuujengea heshima mkoa Mkoa wa Ruvuma

Nao viongozi wa timu ya JKT Mlale na Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoani hapa (FARU) Joseph Mapunda na mwakilishi wa Kikosi cha Mlale Isack Kusimbwa pamoja na neno la shukiurani kwa msaada huo walimuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa watahakikisha timu hiyo inatinga ligi kuu.

Walisema msaada huo umefika wakati muafaka na wakaahidi kufikisha vifaa hivyo kwa walengwa pamoja na salamu zake kwa wachezaji wote na wakatumia nafasi hiyo kumkaribisha kiongozi huyo kushiriki katika michezo hiyo ili aweze kujionea kazi ya vijana wake.
Mwisho

No comments:

Post a Comment