About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, March 24, 2012

VIONGOZI WA MKOA WA MTWARA NA RUVUMA WAASWA KULITA MKONGA WA TAIFA

       Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu
Na Agustino Chindiye,Tunduru
VIONGOZI wa Mikoa ya Ruvuma Mtwara na maeneo yanayopitiwa na Mkongo wa Taifa nchini wameombwa  kuulinda na kuhakikisha kuwa Mkongo wa Taifa haukatwi wala kuhujumiwa kwa njia yoyote ile.

Ombi  hilo  limetolewa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa ambaye anaendelea na ziara ya kukagua Mkongo wa Taifa katika Mikoa ya kusini.

Pamoja na maagizo hayo pia Profesa Mbarawa alitoa elimu juu ya faida za Mawasiliano ya Mkongo wa taifa  kwa viongozi wa Ngazi za Vijiji, Wilaya na hata kwa wananchi wachache kila alipokutana nao kikubwa akihimiza ulinzi wake na kueleza kuwa nyaya zilizo wekwa katika Mkongo huo hazina soko popote Duniani na kwamba atakaye fanya uharibifu wowote atawasababishia wenzake kukosa mawasiliano tu.

Aidha katika hotuba hiyo kwa viongozi hao alisema kuwa mawasiliano kupitia Mkongo wa Taifa yataiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta za Biashara, Uzalishaji mali, Elimu na Afya, pamoja na Ulinzi.

Akizungumzia matatizo ya mawasiliano ya simu za Mkononi yaliyoanza kujitokeza katika siku za Karibuni Prof. Mbarawa alikiri kuwa hali hiyo inatokana na mitambo ya kampuni za simu zilizowekeaz nchini kuwa hivi sasa zimeanza kuelemewa na wingi wa huduma na wateja.

Akifafanua taarifa hiyo Profesa Mbarawa alibainisha kero na matatizo ya simu za Mkononi kutounganishwa vizuri pale mtumiaji anapopiga ama kukoroma, kampuni za Simu kupiga matangazo ya biashara kwanza kabla ya  kumuunganisha mtumiaji anapotaka kuongea na mwingine ama mitambo kutofanya kazi ambayo yamekua yakilalamikiwa na wananchi

Ziara hiyo ya kiukaguzi zaidi, Waziri Mbarawa akipita katika vituo na njia ambazo Mkongo wa Taifa umelazwa kuunganisha mawasiliano kati ya Mkoa na Mkoa ikiwa ni awamu ya kwanza, kabla ya awamu nyingine ambapo wilaya zote pia zitaunganishwa.

Naye Mbunge wa jimbo la Tunduru Kusini ambaye alikuwa mwenyeji wake Abdalah Mtutura alisema kuwa alilazimika kumpeleka Waziri huyo katika Tarafa ya Nalasi ali akajionee maelfu ya wananchi wanaoishi huko huku wakiwa hawana huduma za mawasiliano wala hawasikilizi Radio yoyote ya Tanzania huku ahadi iliyotolewa na Rais kuwa wangejengewa vituo vya kuwawezesha kupata mawasiliano hayo ikiwa haija tekelezwa.

Awali akimsomea taarifa ya maendeleo ya Wilaya hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Juma Madaha alibainisha kuwa mbali na kuwepo kwa utitiri wa makampuni ya simu ya Ttcl.Vodacom, Tigo, Zantel na Airtel lakini huduma hiyo imekuwa ikipatikana kwa uhakika katika makao makuu ya Wilaya na Vijiji vichache.

Alisema Wilaya hiyo ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 18,778 ikiwa na tarafa 7. kata 35 na Vijiji 148 na kwamba ipo umbali wa Kilometa 1264 kutoka jijini Dar es Salaam kupiti makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma Mjini Songea na Kilometa 800 kutoka Dar es Salaam kupitia Masasi Mkoani Mtwara na Mikoa wa Lindi nakuongoza kuwa hali hiyo inapaswa kuangaliwa na serikali katika uimarishaji wa miuondo mbinu yake.
Mwisho


No comments:

Post a Comment