About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, March 22, 2012

DARAJA LASABABISHA KAPTENI KOMBA ASHINDWE KUWAPA POLE WAHANGA

Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba

Na Gideon Mwakanosya, Nyasa
MBUNGE  wa Jimbo La Mbinga Magharibi Kapteni mstaafu John Komba ameshindwa kuendelea na ziara yake ya siku mbili ya kwenda kuwapa pole ndugu wa watu wanao daiwa kuwa wamekufa maji na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya gari waliyo kuwa wakisafiria kutoka Mbinga mjini kwenda kijiji cha Ngumbo kusombwa na maji wakati likiwa linavuka daraja la mto mnywamaji na kusababisha watu wanne kufa maji na majeruhi wawili kufuatia daraja la mto mbuchi kutitia na kusababisha kushindwa kupita magari
Hata hivyo Kapteni Komba alifanikiwa kufika nyumbani kwa marehemu Mwalimu Lucas Godon Mbunda wa kijiji cha Mkili ambako familia ya marehemu pamoja na ndugu na jamaa walikuwa wakiendelea kuomboleza msiba na aliwapa pole na kutoa rambirambi na alitoa ahadi ya kuwalipia ada watoto wawili wa marehemu Mbunda wanaosoma katika shule ya sekondari ya bweni ya Chipole inayomilikiwa na Kanisa la Katoliki  iliyopo wilaya ya Songea vijijini na shule ya sekondari ya Bweni ya Beroya iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Kapteni Komba alifafanua zaidi kuwa analazimika kuchukua jukumu hilo la kuwalipia ada ya mwaka mmoja watoto wa marehemu Mbunda ambao wameachwa wakati mgumu kwani marehemu Mbunda kabla ya kukutwa na umauti alikuwa anatoka Mbinga ambako alikwenda kuhakiki taarifa za akaunti yake ya Benki ya NMB na kuchukua mshahara wake wa mwezi uliopita jambo ambalo limeonesha wazi kuwa watoto hao wanahitaji msaada zaidi wa kulipiwa ada ili waendelee na masomo ambapo fedha zinahitajika Shilingi laki nane kila mmoja .
Kapteni Komba ambaye aliongozana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mbinga wakiwemo Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Anastasia Amasi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Oddo Mwisho aliendelea na ziara yake hadi katika kijiji cha Kihagara ambako alishindwa kuendelea na safari yake baada ya daraja la mto mbuchi kutitia kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha magari kushindwa kupita kwenye daraja hilo.
Wakiwa kwenye eneo la daraja la mto Mbuchi Diwani wa kata ya kihagara (CHADEMA)  Steven Pata alimweleza Mbunge Kapteni Komba  kuwa machi 14 mwaka huu  wakati maafa makubwa yaliyotokea ya vifo vya watu wanne kufa maji na watu wengie kujieruhiwa wakati gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji pia mvua hizo zilisababisha daraja la mto Mbuchi kutitia hivyo aliiomba Serikali ione umuhimu wa kuchukua hatua za haraka za kulitengeneza daraja hilo amabako ni kiungo kikubwa kutoka Liuli na kihagara  na pamoja na wanachi wa kutoka kata za Lihundi, Lundu, Mbaha na Lituhi .
Kwa upande wake Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma Mhandisi Abrahamu Kissimbo alisema kuwa kikosi cha wataalamu wake kimeshafanya tathimini ya uharibifu wa miundombinu uliotokea katika daraja la Mbuchi na kwamba ameahidi kuwa ndani ya wiki mmoja mara tu baada ya kufika vipuli vinavyo hitajika kwenye daraja hilo ujenzi huo utakuwa umekamilika na amepiga marufuku pikipiki na magari kupita kwenye daraja hilo na watakao kamatwa watachukuliwa hatua.
Machi 14 mwaka huu majira ya saaa nane usiku gari aina ya Landlover wanteni yenye namba za usajili T 492 AWY ambalo lilikuwa klikitoka Mbinga kwenda Ngumbo huku likiwa limesheheni abiria pamoja na mizigo lililokuwa likiendeshwa na Bosco Hyera lilisombwa na maji wakati linavuka kwenye daraja la mto Mnywamaji na kusababisha watu wanne kufa maji na watu wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
 Mwisho

1 comment:

  1. Natoa pole sana kwa wahusika wa janga na msiba huu. Mungu awaweke marehemu mahali pema Peponi, na awafariji ndugu, jamaa, na marafiki.

    ReplyDelete