About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, April 19, 2012

GARI NA PIKIPIKI ZAGONGANA NA KUSABABISHA KIFO WILAYANI MBINGA

                 KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMHANDA

NA   DUSTAN  NDUNGURU ,SONGEA.

MTU mmoja mkazi wa Mbinga mjini mkoani Ruvuma amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya gari na pikipiki kugongana katika kijiji cha Makatani.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Maiko Kamuhanda alisema kuwa ajali hiyo imetokea aprili 16 mwaka huu majira ya saa 11.45 katika barabara itokayo Mbinga mjini kuelekea Mpepo.

Kamuhanda alisema kuwa pikipiki aina ya Honda XLR yenye namba za usajili T941 AGJ iliyokuwa ikiendeshwa na Naftari Tweve akiwa amembeba airia mmoja aliyetajwa kwa jina la Yacob Ndunguru imehusika na ajali hiyo.

Alisema kuwa pikipiki hiyo iligongana uso kwa uso na gari aina ya 110 T779 BUU iliyokuwa ikiendeshwa na Saulo Mapunda na kusababisha kifo cha dereva wa pikipiki Naftari Tweve ambaye alifariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Mbinga.

Kamanda huyo alimtaja majeruhi kuwa ni Yacob Ndunguru ambaye alipanda pikipiki na kwamba amelazwa katika hospitali hiyo na hjali yake bado ni mbaya.

                                            MWISHO.

No comments:

Post a Comment