Na Augustino Chindiye,Tunduru
MADIWANI wa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wameibuka na kulilia nyongeza ya
maslahi yao likiwemo ongezeko fidia,nauli na posho za vikao.
Hayo ni miongoni mwa mambo yaliyo ibuka katika kikao cha kawaida cha Baraza la halmashauri hiyo lililo keti katika ukumbi wa Klasta Mjini hapa.
Huku akishangiliwa na Madiwani wenzie katika kikao hicho Diwani wa kata ya Marumba Msenga Said Msenga alisikika akilalama na kuiomba Serikali kutambua na kuona umuhimu wa kuwaongezea mafao pamoja na posho wakati wa vikao.
“Umefika wakati wa Serikali kutuona sisi tunao wawakilisha wananchi ngazi hiyo ya kata maeneo yaliyopo vijijini fedha tunazopata zote zinaishia njiani kutokana na gharama za usafiri na za maisha kuwa juu “ alisema Msenga
Katika taarifa hiyo Diwani huyo alitolea mfano wa madiwani hao kulipwa nauli ya Shilingi 3500 kwa madiwani wanaotoka vijijini lakini wakati huo hali halisi wao hutozwa kati ya shilingi 7,000 na 8,000 kutokana na hali ya maisha kupanda.
Diwani huyo ambaye alionekana wazi kuungwa mkono na madiwani wenzakealifikia hatua ya kupendelezwa kuwa posho zao ziongezeke hadi kufikia shilingi Milioni 3 kutoka Shilingi 120,000 ambazo wamekuwa wakilipwa hivi sasa kwa mwezi.
Mambo mengine yaliyo ibuka katika kikao hicho ni lawama za madiwani hao kwa Serikali wakiituhumu kuchelewesha fedha hali ambayo imepelekea miradi mingi kukwama na kusababisha kero kwa wananchi.
Akifafanua kero hiyo Mtoaji wa kero hiyo Makamu mwenyekiti wa halamashauri ya Wilaya hiyo Diwani wa kata ya Nakayaya Charles Haule alisema kuwa pamoja na kukiweka chama tawala katika wakati mgumu katika chaguzi zijazo.
Alima pamoja na hali hiyo pia hivi sasa asilimia kubwa ya wananchi imeonekana kukatishwa tamaa na utendaji wa viongozi waliopo madarakani kutokana na kushindwa kusimamia maendeleo na kufanya miundombinu hasa ya barabara kushindwa kupitika wakati wote wa mwaka.
Hata hivyo Haule alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani wenzake kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi ili waongeze juhudi za kushiriki katika shughuli za kimaendeleo tofauti na sasa ambapo wamekuwa wakigoma kufanya kazi hizo wakiamini kuwan miradi yote imekuwa ikitengewa fedha za kutosha kutekeleza miradi hiyo kwa asilimia 100.
Awali akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo alikiri kuwepo mrundikano wa mirani viporo hali iliyoonesha kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa fedha za miradi kutoka Serikali kuu.
Mwisho

No comments:
Post a Comment