About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, April 23, 2012

MBARONI KWA KUBAKA NA KUMWEKA MIMBA BINTI WA MIAKA 17

KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMHANDA

Na Gideon Mwakanosya, Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Baraka Makeo (19) mkazi wa eneo la Chandamali katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka kumi na saba mkazi wa Bombambili ambaye jina lake limehifadhiwa kinyume na sheria.
Akizungumza na www.stephanomango.blogspot.com  jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitoke April 16 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni huko katika eneo la Bombambili mjini hapa.
Alisema inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio msichana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alikutwa akiwa amewekwa kinyumba  na mwanaume huyo Makeo baada ya kutafutwa kwa muda mrefu na wazazi wake ambao wanadai kuwa aliondoka nyumbani kwao kwa mazingira ya kutatanisha na hawakujua alipoelekea tangu wiki moja iliyopita.
Alifafanua zaidi kuwa taarifa ya kuto kuonekana kwa msichana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa ilishatolewa katika kituo kikuu cha Polisi cha Songea mjini na Polisi  kwa kushirikiana na ndugu huyo waliendelea kumtafuta hadi april 16 mwaka huu alipokutwa amewekwa kinyumba na mtuhumiwa Makeo.
Alieleza zaidi kuwa baada ya msichana huyo kukutwa nyumbani kwa Makeo Polisi iliamua kumchukua na kumpeleka katika Hospitali ya mkoa ya Songea kwa uchunguzi zaidi ambako iligundulika kuwa msichana huyo ana mimba ya miezi mitano ambayo inadaiwa kuwa alipewa na mtuhumiwa .
 Kamanda Kamuhanda alifafanua zaidi kuwa mtuhumiwa Makeo anatarajiwa kufikishwa Mahakamani mara tu upelelezi wa tukio hilo utakapo kamilika .
Mwisho.

No comments:

Post a Comment