About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, April 16, 2012

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA KUJENGA STENDI YA KISASA KWA BILIONI 1.5

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA ODDO MWISHO

NA DUSTAN  NDUNGURU   MBINGA.

HALMASHAURI ya wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma,imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mabasi na majengo mawili yatakayotumika kwa ajili ya maduka kwa wafanyabiashara wilayani humo.

Akizungumza wakati wa utiliaji saini kati ya halmashauri hiyo na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kampuni ya GNMS kutoka mkoani Iringa,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Oddo Mwisho alisema licha ya kujenga eneo la kuegesha magari lakini kutakuwa na majengo mawili yatakayokuwa na maduka.

Alisema kuwa lengo la kufanya hivyo  ni kuongezeka kwa  mahitaji  ya wananchi wa wilaya hiyo hasa wale wenye vyombo vya moto ambao wamekuwa wakipata shida ya kuegesha magari yao pindi wanapotaka kuingia kituoni hapo,na mahitaji mengine yakiwemo ya maeneo ya kufanyia biashara.

Mwisho alisema mkataba wa ujenzi wa kituo hicho cha mabasi unalenga kuboresha huduma za usafiri,usafi na hata ulinzi kwani hapo mwanzo ilikuwa ni kazi ngumu kufanya vitu hiyo kutokana na eneo ilo lilivyo hasa baada ya kuongezeka kwa idadi ya magari.

Kuhusu fedha za mradi huo alisema kuwa fedha ziko tayari na kwamba kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa ili hatimaye iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa.

Alifafanua kuwa fedha za mradi huo zimepatikana  kutoka mfuko wa kuzipatia ruzuku halmashauri, chini ya wizara ya  serikali  za mitaa(TAMISEMI)ambayo imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1.3 na kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 200 ni fedha za halmashauri yenyewe  kutokana na mapato yake ya ndani.

Pia aliongeza kuwa halmashauri ya wilaya ya Mbinga imejipanga katika utekelezaji wa ahadi za chama cha mapinduzi(CCM) ilizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu  mwaka 2010 kuwa itajenga kituo kipya cha mabasi na kuboresha baadhi ya maeneo muhimu yakiwemo hospitali zake zote,barabara za mitaa na huduma ya maji.

Juu ya mkakati wa kuongeza mapato ya halmashauri Mwisho alisema wamejipanga vizuri na  hamashauri ya mbinga imeshaanza kuchukua hatua kwa kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa mahoteli na imeshatuma baadhi ya wataalam wake kwenda mkoani Mbeya  kuangalia michoro ya soko la kisasa la Mwanjelwa ili nao wajenge soko linaloweza kufafanana na ilo kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi kuiongeza vitega uchumi kwa halmasghauri yao.

Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shaibu Nnunduma aliwaomba wananchi wa mbinga kutunza miradi hiyo ambayo ipo kwa faida yao na kuona kuona umuhimu wa kuitunza ili kufanikisha kazi iliyokusudiwa kwa ajili ya  kuiletea halmashauri  fedha nyingi zitakasaidia kuboresha hudunma za jamii katika wilaya hiyo.

Alisema miradi hiyo inagharimu kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni za kwao hivyo kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa inatunzwa na kwamba wawe macho na watu wenye tabia ya kuhujumu.

                         MWISHO.

No comments:

Post a Comment