Na Steven Augustino, Tunduru
WAKULIMA wa Mpunga Wilayani Tunduru wametakiwa kuukataa kuuza mpunga wao kupitia mfumo wa Stakabadha gharani na kugoma kulipa ushuru kulingana na maelekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya wilaya hiyo .
Pamoja na wito huo wakulima wa mazao hayo pia wamehimizwa kuwa na mshikamano wa kugomeaa tozo za ushuru ambao umedaiwa kutozwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo hata kwa wakulima wanao ingiza mazao yao kutoka shambani.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Viongozi waandamizi wa Chama cha wananchi CUF wa Wilaya ya Tunduru kwa ushirikiano wa viongozi wa chama hicho kutoka Mkoani Mtwara wakati wakiongea na wananchi katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya baraza la Idd mjini hapa.
Akifafanua hotuba hiyo Mgeni rasmi katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha wananchi Cuf Wilaya ya Tandahimba na Mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 Katani Mohamed alisema kuwa ukosefu wa wataalamu wabunifu na uvivu wa kujituma kwa viongozi katika halmshauri hiyo ndiko kuliko wasukuma kuandaa utaratibu huo huku
wakifahamu wazi kuwa mpango huo unalenga kuwaibia wakulima hao.
wakifahamu wazi kuwa mpango huo unalenga kuwaibia wakulima hao.
Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo Katani aliwahimiza kudai haki zao bila kuogopa jambo lolote kwani vitendo hivyo vya unyonyaji ni hatari kwa ustawi wa jamii
Katani aliendelea kueleza kuwa kinachowafanya viongozi hao kufikia hatua hiyo ya kuchukua maamuzi bila kuwashirikisha wananchi kinatokana na wanatunduru wenyewe kulala usingizi wa pono na akatumia nafasi hiyo kuwataka waamke kudai haki zao vinginevyo watajikuta wameuzwa katika maeneo yao.
Alisema wakati viongopzi hao wakifikilia kuingiza zao hilo katika mfumo huo viongozi hao bado wameendelea kuwa kero katika utoaji wa msaada kwa wakulima wakorosho ambao pia waliingizwa katika mkenge huo bila kuwepo kwa makubaliano.
Akizungumzia tozo kwa wakulima wa mpunga alisema ingawa viongozi hao wanafahamu maelekezo na miongozo ya tozo hizo iko wazi kuwa anayetakiwa kulipa ushuru ni mtu yeyote au mfanyabiashara anayeondoka na shehene ya chakula kutoka ndani ya wilaya husika.
Wakitoa salamu kutoka mkoani Mtwara Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Cuf Taifa Reherma Mautuka, Katibu wa Cuf Wilaya ya Tandahimba Shaban Namaneha,Katibu wa Cuf Mtwara Mjini Said Mdoya na Mkurugenzi wa haki za binadamu Wilaya ya Tandahimba Alfonce Andrew walisema kuwa mikikimikiki ambayo imekuwa ikijitokeza katika Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara imetokana na kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji kutoka kwa viongozi wao.
Awali akimkaribisha msemaji mkuu katika mkutano huo mwenyekiti wa CUF
Wilayani humo Abdalah Mtalika alidai kuwa kitendo cha kuwatoza wakulima Ushuru huo wakati wakiingiza mazao yao kutoka Shambani ni cha uonevu kwavile wakazi wote wa mji huo hulima vijijini.
Mwisho
No comments:
Post a Comment