Mjumbe wa Bodi ya Muunganiko wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Mhariri Msaidizi wa Kanda ya Kusini(Tujifunze) na Mhandishi wa Habari wa Uhuru Fm, Juma Nyumayo akitoa mada ya mchango wa vyombo vya habari katika jamii katika mdahalo ulioandaliwa na Kituo cha Redio Jogoo Fm siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Mei 3
Mwandishi wa Serikali za Mitaa Tanzania mkoani Ruvuma(ALAT) Mwakilishi wa Vyombo vya IPP MEDIA(Nipashe,Guardian,Redio One na Itv) Nathan Mtega akizungumza katika Studio ya Kituo cha Redio Jogoo kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari katika maendeleo ya Jamii, katikati ni Muongozaji wa kipindi hicho Isabela Nchama,wa kwanza kulia ni Aden Mbelle ambaye alikuwa ni msimamizi wa kipindi hicho
Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Dira ya Mtanzania, Changamoto,Mitandao mbalimbali ya Kijamii na mmiliki wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com, Stephano Mango akitoa mada ya umuhimu wa vyombo vya habari katika kukuza Demokrasia nchini, kulia ni Msimamizi wa kipindi Aden Mbelle
Kutoka kushoto ni mwongozaji wa kipindi hicho kilichorushwa hewani moja kwa moja na kituo cha Redio Jogoo Fm, Isabela Nshana na Aden Mbelle ambaye alikuwa msimamizi wa matangazo hayo siku ya uhuru wa vyombo vya habari mei 3 mwaka huu
Mtangazaji wa Redio Jogoo Innocent akifanya mahojiano na Mwandishi Juma Nyumayo katika Studio ya Redio hiyo siku ya Uhuru wa vyombo vya habari
Mtangazaji wa Redio Jogoo Innocent akifanya mahojiano na Mwandishi Nathan Mtega katika Studio ya Redio hiyo siku ya Uhuru wa vyombo vya habari mei 3, katikati ni Mwandishi Juma Nyumayo
Mwandishi Nathan Mtega akisaini kitabu katika Studio ya Redio Jogoo Fm ikiwa ni ishara ya kumaliza kipindi kilichorushwa moja kwa moja na Redio hiyo, kushoto ni Mtangazaji wa kituo hicho Isabela Nshama siku ya uhuru wa vyombo vya habari mei 3 mwaka 2012
Mwandishi Juma Nyumayo akiteta jambo na Mtangazaji wa Redio Jogoo Fm Aden Mbelle baada ya kumaliza mdaharo wa umuhimu wa vyombo vya habari katika muktadha wa uchumi, siasa na utamaduni
MUDA WA TAFRIJA KATIKA UKUMBI WA SONGEA CLUB MAMBO YALIKUWA HIVI............
Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama mbaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kuwa mgeni rasmi katika tafrija ya jioni ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Ruvuma, kushoni ni Katibu Mtendaji wa Chama cha waandishi wa habari moani Ruvuma Andrwe Chatwanga, wapili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Andrwe Kuchonjoma wakiimba wimbo wa kuisifu na kuipenda TANZANIA
Katibu Msaidizi wa Ruvuma Press Club, Mozes Julius Konala na Mwandishi wa Tanzania Daima kushoto, kulia ni Mwekahazina Msaidizi na Mwandishi wa Channel Ten mkoani Ruvuma Emmanuel Msigwa wakiimba wimbo wa kuipenda TANZANIA
Waandishi wa habari kutoka kulia ni Jofrey Nilai Redio Maria na Mjumbe wa Kamati wa Ruvuma Press Club, Mwakilishi wa IPP MEDIA mkoani Ruvuma Nathan Mtega na Anna wakiimba wimbo huo
Mwandishi wa Jambo Leo Thomas Lipuka Komba akitoa maombi kwa niaba ya dhehebu la kikristo katika tafrija hiyo
Naye akitoa maombi kwa niaba ya dhehebu la kiislam
Hongereni kazi nzuri unayoifanya na nimefurahi kuona kila kitu kimeenda safi. PAMOJA DAIMA...
ReplyDelete