About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, May 17, 2012

RC ENG, MANYANYA AKEMEA MAUAJI YA KISHIRIKINA RUKWA

 Na Elizabeth John, Rukwa
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya,  amekemea kushamiri kwa vitendo vya mauaji  ya imani za  kishirikina vinavyofanywa na baadhi ya watu.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu juzi, alisema matukio hayo ambayo yamepoteza maisha ya watu kadhaa katika kipindi cha miaka miwili sasa, yamechangiwa na wakazi wengi wa vijiji mbalimbali mkoani humo kuamini uchawi.

Manyanya aliongeza kuwa matukio hayo yamekuwa yakiufedhehesha mkoa huo lakini pia yamerudisha nyuma jitihada za baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kujitafutia maendeleo yao.

“Hali hii si nzuri kwani wengi wameuawa kutokana na wivu wa baadhi ya wakazi wenzao ambao wamekuwa wakishuhudia maendeleo ya kasi na mwisho wa siku wanawazushia uchawi, jambo ambalo si la kweli,” alisema Manyanya.

Alisema kuwa wanaofanya vitendo hivyo vya mauaji hawana tofauti na wahuni wengine wasiopenda maendeleo ya wanakijiji wenzao.

Kumekuwa na matukio mengi ya mauaji yanayotokana na imani za kishirikina ambapo wiki mbili zilizopita, wazee wawili wa Kijiji cha Miangalua wilayani Sumbawanga waliuawa sanjari na nyumba 42 kubomolewa na kuchomwa moto.

Katika tukio hilo pia wanakijiji waliteketeza mifugo mingi, kutokana na hasira za wenzao kumtuhumu mwanakijiji huyo kumroga kijana  mmoja, Festo Chambanenge, ambaye alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment