About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, May 16, 2012

Yeah: Sasa ni Undava Undava tu! [WANAFUNZI WAASI, MKUU WA SHULE ANUSURIKA KUUAWA)


Yeah: Sasa ni Undava Undava tu! [WANAFUNZI WAASI, MKUU WA SHULE ANUSURIKA KUUAWA) LOL

MKUU WA SHULE ANUSURIKA KUUAWA

Katika tukio lingine, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Muhoro iliyopo Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani, ameponea chupuchupu kuuawa na wanafunzi baada ya kukimbilia porini akikwepa kipigo kutoka kwa wanafunzi wapatao 400.
...

Vurugu hizo zilitokea jana asubuhi baada ya wanafunzi hao kuasi na kuzingira shule kabla ya kufunga barabara itokayo Dar es Salaa kwenda Mtwara na kusababisha abiria kukwama kwa muda.

Kwa mujibu wa shuhuda mmoja, wanafunzi hao walikuwa wanamtuhumu mwalimu wao aliyejulikana kwa jina moja la Mwita, kuwa anawalisha ugali na maharage kila siku pamoja na kushindwa kuwapa tisheti za shule licha ya kuwa wamezilipia.

Wanafunzi hao pia wanamtuhumu mwalimu huyo kwa kushindwa kuandaa mikakati ya kuwawezesha kushiriki katika michezo ya shule pamoja na kushindwa kuwapatia vitambulisho vya shule.

Shuhuda huyo alisema mwalimu huyo baada ya kuona wanafunzi wameasi na kuanza kuzingira eneo la shule, alikimbilia porini kukwepa kipigo.

Kutokana na vurugu hizo, wanafunzi wawili walijeruhiwa na hali zao ni mbaya, huku wengine 12 wakiwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika wilayani Rufiji.

Taarifa kutoka eneo la tukio zilisema kuwa, baada ya abiria ambao magari yao yalizuiwa kupita walishuka na kuanza kushirikiana na polisi kuwaondoa wanafunzi hao barabarani.

Mapambano hayo yalikuwa makali baada ya wanafunzi kuanza kuchukua mawe kutoka barabarani na kuanza kuwapiga abiria, ambapo baada ya kuzidiwa walikimbilia vijijini kujificha.

Vurugu hizo zilisababisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, kufika eneo la tukio na kufanya kikao cha dharura jana jioni, ambapo aliahidi kushughulikia kero za wanafunzi hao haraka na kuzipatia ufumbuzi.

Mahiza akizungumza na NIPASHE jana jioni alithibitisha kwenda eneo la shule hiyo kutafuta suluhu ya vurugu hizo.

Mahiza alisema vurugu hizo zilimalizika na kwamba ameuagiza uongozi wa wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya kushughulikia madai ya wanafunzi hao.

Hata hivyo, Mahiza alisema wanafunzi hao walikuwa na hoja, lakini hawakuwa na sababu ya kufanya vurugu na kufunga barabara.

“Hawa wanafunzi kufunga barabara na mgogoro wao na uongozi wa shule kuna uhusiano gani kama siyo ukorofi wa wanafunzi?” alihoji.

Alisema wanafunzi wanane wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano ili kubaini vinara walioanzisha vurugu hizo.

Imeandikwa na Emmanuel Lengwa, Rungwe; Ashton Balaigwa, Ulanga na Richard Makore, Dar.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment