About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, June 23, 2012

WASAFIRISHAJI RUVUMA WAIDAI SERIKALI ZAIDI YA MILIONI 375

Na Stephano Mango, Songea
WASAFIRISHAJI wa Mizigo mkoani Ruvuma wameitaka Serikali kupitia  Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika kuona umuhimu wa kuwalipa deni la fedha zaidi ya milioni 375 wanazozidai kwenye kitengo cha Taifa cha kuhifadhi mahindi kilichopo mkoani Ruvuma (SGR) baada ya kufanya kazi ya kubebelea mahindi kutoka vijijini na kuyaleta kwenye hifadhi hiyo mwaka 2011
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wasafirishaji hao ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa walikopwa kuyabebelea mahindi hayo kwa ahadi kuwa fedha zao wangelipwa mara baada ya kumaliza kubebelea na kuyaleta kwenye hifadhi lakini cha ajabu toka wamemaliza kuyaleta mahindi hayo ambayo tayari yameuzwa na Serikali hawajalipwa hali ambayo inaendelea kuwakatisha tamaa
Walisema kuwa wafanyabiashara wengine waliikodisha Serikali Magodauni ili wahifadhi mahindi hayo kwa sababu Magodauni ya kituo cha Hifadhi kilichopo mjini hapa hayakuwa na uwezo wa kuhifadhi mahindi yaliyokuwa yanabebelewa na wasafirishaji kutokana na uwingi wake, pia wapo wafanyabiashara ambao walikopwa mafuta lakini wote hawajalipwa
Walisema kuwa Wasafirishaji hao walijitahidi kwa uaminifu mkubwa kuyabebelea mahindi hayo kutoka kwenye maeneo ambayo miondombinu yake ni mibovu sana huku mafuta na vipuri vya magari vikipanda kila mara hivyo tumepata tabu sana na sasa biashara zetu zinayumba tunaiomba Serikali itulipe fedha zetu
Walieleza kuwa wafanyabiashara hao wana mikopo ya biashara Benki na wanalipa kodi mbalimbali zikiwemo za Mamlaka ya Mapato (TRA) na wanachangia michango mbalimbali ya maendeleo mkoani hapa lakini wanashangazwa na kitendo cha Serikali cha kutowathamini wasafirishaji hao kwa kuwacheleweshea fedha zao hali ambayo inasababisha kupungua kwa mzunguko wa fedha mkoani Ruvuma na kupungua kwa kasi ya ulipaji wa kodi kutokana na madeni wanayodaiwa
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoani Ruvuma Mays Mkwembe alisema kuwa wafanyabiashara wengi ambao waliikopesha Serikali ili kuweza kufanikisha uletaji wa mahindi mjini wamekuwa wakihangaika sana katika shughuli zao kutokana na fedha nyingi kuidai Serikali
Mkwembe alisema kuwa ni vema Serikali ikawalipa wafanyabiashara haraka ili waweze kulipa kodi ambazo wanadaiwa katika msimu wa fedha wa 2011/2012 kwani bila kufanya hivyo hali ya mapato ya mkoa yatakuwa ni madogo sana kuliko ilivyopanga, ingawa pia wafanyabiashara wengi wanadaiwa riba kwenye taasisi za fedha kutokana na mikopo waliyoikopa
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko alikiri kuwa wafanyabiashara wanaidai Serikali kutokana na huduma waliyoitoa hivyo wasubiri kidogo kwani Serikali inaandaa utaratibu wa kuwalipa haki zao kama ambavyo makubaliano yalivyo kwani Serikali inatambua mchango wao katika harakati za kimaendeleo mkoani hapa na taifa kwa ujumla.
MWISHO

No comments:

Post a Comment