About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Tuesday, April 23, 2013

MKIA MIWILI YA TEMBO YAMSABABISHIA KUSHIKILIWA NA POLISI RUVUMA

Na Gideon Mwakanosya,Songea.


JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wa tano kwa matukio tofauti likiwemo la watu wawili kukamatwa na mikia miwili ya Tembo ,Risasi tatu na kichwa kimoja cha bunduki aina ya Rifle huku tukio la pili ni mtu moja kukamatwa na bangi kilo 50 na miche ya bangi yenye uzito wa kilo 62 wakati tukio la tatu yote ya wizi wa pikipiki huku pikipiki mbili ziliibiwa jijini Dare-Esalaam na moja ya mjini Songea mkoani Ruvuma.

Watuhumiwa wanaoshikiliwa na polisi katika matukio matatu tofauti ni Rashidi Kapesa [29] Teofanesi Mapunda [29] Eleneus Mapunda [37] Bakari Milanzi [40] na Yahaya Rajabu umri wake haukutajwa

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimeki alisema kuwa tukio la kuwakamata watuhumiwa na mikia ya Tembo lilitokea Aprili 18mwaka huu majira ya 1.30 jioni baada ya askari wanyama pori Hassani Mihuka alipokuwa doria na wenzake waliwakamata Rashidi Kapesa [29]mkazi wa kijiji cha Mandepwende na Teofanesi Mapunda [29]mkazi wa kjiji cha Mtonya .

Kamanda wa polisi alisema kuwa watuhumiwa hao waliokamatwa eneo la kambi ya watu wakujenga barabara Progressive lililopo Mchomolo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ambao walikutwa na mikia 2 ya Tembo ,Risasi 3 kichwa kimoja cha bunduki aina ya Rifle kilichokuwa kimefichwa ndani ya begi.

Kamanda Nsimeki alisema kuwa mnamo Aprili 20 mwaka huu mjira ya saa kumi jioni huko katika kijiji cha Ngahokola mashambani wilayani Songea ambako askari polisi wakiwa kwenye doria yao ya kila siku walifanikiwa kumkamata Eleneusi Mapunda akiwa na bangi kiasi cha kilo 50 na miche ya bangi yenye uzito wa kilo 62.

Alifafanua zaidi kuwa katika tukio lingine inadaiwa kuwa mnamo Marchi 7 mwaka huu katika muda usiofahamika kwenye eneo la Lizaboni manispaa ya Songea polisi ilifanikiwa kumtia mbaloni Bakari Milanzi [40]aliwa na pikipiki yenye namba za usajili T354 BNZ SANLG na baada ya uchunguzi yakinifu ilibainika kuwa namba halisi za usajili wa pikipiki hiyo ni T 775 BWC mali ya Teodora Sephan Mtweve wa jijini Dare –Esalaam ambaye inadaiwa pikipiki yake iliibiwa tangu mwezi Julai 2012 katika eneo la Kimara baada ya mwendesha bodaboda huyo kuporwa na mtu asiye fahamika.

Kanda alilitaja tukio lingine kuwa inadaiwa mnamo Marchi 7 nwaka huu askari polisi walio kuwepo eneo la doria la Lizaboni manispaa ya Songea mtuhumiwa Yahaya Rajabu alikamatwa na pikipiki yenye namba za usajili T 557 BYR aina ya SANLG ambayo baada ya kufanya uchunguzi ilibainika kuwa namba zake halisi za usajili kuwa ni T 7551 BSY ambayo mmiriki wake halisi ni Rose Gerevas Makene mkazi wa jijini Dare –Esalaam ambaye pikipiki hiyo iliibiwa katika maeneo ya Kimara Julai 7 mwaka 2012 baada ya mwendesha bodaboda huyo kuporwa na watu wasiofahamika.

Aidha alilitaja tukio jingine kuwa mnamo Februari mwaka huu khuko katika wilaya ya Tunduru askari wakiwa kwenye doria walifanikiwa kukamata pikipiki yenye namba za usajiri T.736 aina ya SANLG ambayo baada ya polisi kufanya uchunguzi wa kina ilibainika kuwa namba hizo kuwa ni bandia hivyo namba halisi za usajili wa pikipiki hiyo kuwa ni T 787 CDL na kuwa ni mali ya Isdori Mdolino mkazi wa Songea mjini ambayo inadaiwa iliibiwa Januari 26 mwaka huu. na baada ya mwendasha bodaboda kuporwa na kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakani mara baada ya upelelezi kukamilika.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment