Sunday, April 28, 2013
RC MANYANYA APEWA TUZO YA HESHIMA TANZANIA
Mbunge wa Viti Maalum (Ccm) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Na, Stephano Mango, Songea
WAFANYAKAZI wa Sekta mbalimbali Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamelipongeza Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi, Viwandani, Biashara, Taasisi za fedha, Huduma na Ushauri Tanzania (Tuico) kwa kitendo chake cha kuwatunuku vyeti vya uanachama wa Heshima baadhi ya wadau muhimu wa chama hicho akiwemo Mbunge wa Viti Maalum (Ccm) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com walisema kuwa katika nchi hii kuna baadhi ya Viongozi wanathamini sana juhudi za Wafanyakazi waliopo katika sekta mbalimbali kwa kuwashauri, kuwatia moyo na kushiriki kuyatatua matatizo yanayowakabili
Walisema kuwa Mhandisi Manyanya amekuwa kinara wa kuwatetea wafanyakazi toka alipokuwa anafanya kazi katika Shirika la Tanesco, hadi sasa akiwa katika nafasi ya Mbunge na Ukuu wa Mkoa wa Rukwa,
“Katika shughuli za kuwatetea Wafanyakazi kwa dhati ili aweze kujenga mshikamano zaidi katika Chama cha Tuico wanachama na Kamati mbalimbali waliamua kumchagua kuwawakilisha kwenye shughuli mbalimbali zitakazo sababisha maslahi bora ya wafanyakazi nchini” walisema
Walifafanua kuwa tuzo iliyotolewa inaheshimika sana katika Tuico kwani inatambua na kuthamini mchango wa mtu, uzoefu, busara, uamuzi, wa haki uliokifanya chama hicho kiweze kuendelea na kuwa na umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama katika mambo mengi ikiwemo kutetea maslahi ya wafanyakazi ambao kimsingi ndio wanachama
Akizungumza kwa njia ya simu mara baada ya tafrija iliyofanyika Morogoro Mjini katika ukumbi wa Midland Inn, kuwatunuku wanachama Tuzo za heshima Mwenyekiti wa Tuico Taifa Omary Ayubu alisema kuwa chama chake kitakuwa kimekosa shukrani kwa wanachama wake ambao wametumia nguvu kubwa ya kutetea maslahi ya chama toka wamekuwa wanachama katika chama hicho
Ayubu alisema kuwa chama kimethamini na kitaendelea kuthamini ujuzi na juhudi walionao wanachama hao waliopewa tuzo katika kukiendeleza chama ili kiwe na tija kwa jamii ambayo inaitumikia na pia kwa maendeleo mapana ya Taifa
“Tumefanya hivyo baada ya kujifunza kwenye Mataifa ya wenzetu kama vile Zambia, Nigeria, Uholanzi, Ivory Cost, Afrika ya Kusini ambapo chama kimekuwa kikijisahau na kuepusha migogoro ikiwamo ya ndani na nje hivyo juwa tegemeo na heshima kubwa” alisema Ayubu
Aliwataja Wanachama hao ambao waliotunukiwa vyeti vya heshima na kupewa tuzo ni pamoja na Rc wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya(Mb), Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Kitivo cha Sheria Profesa Issa Shivji, Felista Bulaya, Barozi Afred Tandau, Wakili Julius Bundala, Zephania Sumbe
Alizitaja majukumu ya wanachama mara baada ya kutunikiwa tuzo hizo kuwa ni pamoja na kushauri knuu8ongozi mambo ya kimaendeleo, kushiriki kampeni za kuelimisha jambo lolote linalohusu chama, kushiriki mikutano na kutoa michango, kutatua migogoro ya kichama, kujenga misimamo ya kichama na kuwakilisha jambo lolote ambalo chama kinataka kwa wakati wowote
Akizungumza kwa njia ya simu kwa niaba ya wanachama ambao wamebahatika kupata tuzo hizo za Mhandisi Stella Manyanya alisema sekta isiyo rasmi ya ajira ina zaidi ya watanzania milioni moja wanaohitaji kujengewa msingi imara juu ya haki zao za msingi ikiwamo mishahara na marupu rupu yanayokwenda sambamba na hali ya maisha
Manyanya alisema kuwa muda umefika sasa kwa vyama vya Wafanyakazi nchini kutumia tafiti na hesabu zilizotafitiwa kwa kina na kubainisha faida na hasara ili wanapoamua kudai haki zao waweze kusikilizwa kwa kina na madai yao kutafutiwa ufumbuzi na waajiri badala ya kukalia kubishana na kuburuzana mahakamani
Alisema kuwa wanachama wa Tuico wanapaswa kwa dhati kabisa kuzitambua haki zao za utumishi na kwamba Waandishi wa habari na vyombo vyao nchini kushiriki kikamilifu kukabiliana na changamoto zinazowakabili wafanyakazi hususani walioko kwenye sekta isiyo rasmi ili waweze kusaidia na uongozi uliopo
MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment