Thursday, July 4, 2013
MAMBO 10 YA MUHTASARI WA ZIARA YA RAIS OBAMA BARANI AFRIKA
Ametusemea Waafrika wote. Hasa katika swala la kujenga viwanda hapa hapa Afrika ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wetu. Africa tusikubali kudanganywa kwa kuuza malighafi kwenda nje na kuhamishia ajira nchi za nje.
Amekemea sana swala la uongozi mbaya, rushwa, upendeleo katika swala la ajira kuwa vinakwamisha maendeleo Afrika.
Yeye na Rais wa Afrika Kusini, wamezungumzia swala la ICC na Afrika. Walisema kama Afrika inafikira kuwa ICC inaionea, ni bora Afrika izungumze na ICC. Lakini Rais Obama alitoa angalizo kwa viongozi wa Afrika kwa makini na madai yao ndani ya ICC.
Hapa Afrika kusini, alizungumzia swala la uchafuzi wa anga na hatua ambazo Marekani inachukuwa kupungaza hatari hiyo. Pia alielezea hatua ambazo China, India na Japan wanachukuwa. Alishauri kila mtu, watu na nchi wote tuhusike na swala hii la uchafuzi wa anga na maeneo tunayo ishi.
Alizungumzia, idadi ya wanafunzi darasani. Alisikitika kusikia kuwa darasa moja Afrika lina wanafuzi 90, ambapo Marekani dalasa moja lina wanafunzi 25 hadi 35 ambao bado waonaona ni wengi. Alishauri kuwepo utalaamu wa kisasa wa kufundishia darasa vikundi vikundi.
Aliwapa changamoto vijana wote wa Afrika ya kusoma sana hasa masomo ya hesabu na ufundi, kuwa tayari kwa ajira za viwandani. Aliahidi kuwapa msaada wa elimu kwa swala hili.
Aliwaambia vijana kuwa tayari kuwania nafasi za juu serikalini na kuwajibisha serekali zao kwa njia za amani.
Alikanusha uvumi uliopo kuwa anataka kuweka kituo cha Jeshi Africa. Pia safari ya Afrika hakusababishwa na uhusiano wa China-Afrika.
Amesema Afrika itajengwa na Waafrika kwa faida ya Afrika wote, ila wao wako tayari kuchangia mawazo, utalaamu na soko.
Aliwajibu Wakenya kuwa ahadi ya kuwatembelea bado ipo pale pale, maana bado ana miaka 3 na miezi 6 ofisini.
Ahsante.
Samuel G Mossama
Pretoria
+27 782 372 288
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment