|
Friday, September 20, 2013
WAZIRI AMTISHA JK
Thursday, September 19, 2013
WAANDISHI WAKWIDWA , WANYANYASWA NA KUPOKEA KIPIGO
Friday, September 13, 2013
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania ( TGNP) U ssu Mallya
Na,Alpius Mchucha—Namtumbo
BAADHI ya wanawake wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,wamesema
wangetamani siku moja kuona katika katiba ijayo kunakuwa na kipengele
maalum cha kuwabana wanaume wanaowakashifu wanawake kwa kutaja sehemu za siri
za wanawake hao kwani tabia hiyo imekuwa ikiwadhalilisha sana kwa jamii na
kuwavunjia heshima na utu wao.
Wakizungumza katika mdahalo wa siku moja jana uliowakutanisha wanawake
zaidi ya 50 kutoka katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo wanawake hao
walisema,wameshachoshwa na matusi yanayotolewa na wanaume ambayo yanataja
sehemu za mwili wa mwamke hivyo ni lazima kutafuta njia ya kukomesha
kwakuwa matusi hayo yamewafanya kuonekana kama siyo watu wanaotoa mchango kwa
jamii na nchi.
Mdahalo huo wenye lengo la kujadili,kubadilishana uzoefu, kujifunza masuala
ya kijinsia na elimu ya uraia uliandaliwa kwa pamoja na shirika
lisilokuwa la kiserikali la Oxfam na mradi wa kuwawezesha vijana wa Restless
Devolopment ulifanyika katika ukumbi wa Parokia mjini Namtumbo.
Mmoja wa wanawake hao Christina Kuhimini alisema, sasa wameshachoshwa
na udhalilishaji dhidi yao hivyo kuiomba serikali kutokuwa na
huruma na watu hao wasiokuwa na hata chembe ya aibu ambao kila
kukicha wanatafuta maneno mapya ya kuwakashifu wanawake licha ya kutambua
kuwa bila ya mwanamke basi hata wanaume hao wasingeweza kutokea
hapa Duniani kwa kile alichoeleza kuwa hakuna binadamu anayeweza kuzaliwa na
mwaume bila ya kuwa na mwanamke.
“bahati mbaya sana muda wa kutoa maoni kwa ajili ya katiba mpya
umekwisha,lakini kupitia vyombo vya habari vilivyopo hapa leo naomba sana
watufikishie ujumbe wetu sisi wanawake wa Namtumbo tumechoshwa sana na matusi
yanayotolewa na wanaume kila siku,tena ni mibaba mizima nayo utoa lugha za
kuwakashifu wanawake ambao hawana hatia yeyote,ili siyo jambo jema hata kidogo
ni baya linalowadhalilisha wanawake”alisema.
Aliongeza kuwa, tabia hiyo ya matusi licha ya kutaja maumbile
ya ndani ya mwanamke lakini kwa bahati mbaya sana imekuwa ikiwarithisha watoto
wadogo wanaohitajki kusikia au kufundishwa matendo mazuri kutoka kwa watu
wazima,lakini cha kushangaza hakuna hatua inayochukuliwa hivyo kuendelea kuota
mizizi na kuonekana kama jambo la kawaida.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake na mratibu
wa dawati la jinsia mkoani hapa Mrakibu wa jeshi la polisi Anna Tembo
alisema tatizo kubwa lililopo ni wazazi kushindwa kuwafundisha maadili
mema watoto wao tangu wakiwa wadogo hivyo kujikuta wakiiga tabia mbaya za
mitaani ambazo hazina misingi bora kwao.
Pia amewataka wanawake kubadilika na kuanza kujitambua kwa kutojihusisha
katika matukio yanayowafedhehesha ambayo yanawafanya kuonekana vituko kwa jamii
ya kistaarabu na ambayo kwa kiasi Fulani yanawapa kiburi wanaume kufanya watakalo
kwa wanawake.
Tembo alieleza kuwa,wanawake wengi wanafanya matukio ambayo
ndiyo yanayowapa hamasa wanaume kufikiria kuwa mwanamke ni chombo cha kutumika
vibaya badala ya pambo ndani ya nyumba na kuendelea kuwafanyia unyama wa kila
aina akina mama.
Alitaja uvaaji wa nguo fupi, zinazobana na zinazoonesha maumbile
yao,kucheza shoo nyakati za usiku katika sehemu za starehe,kujiuza, na hata
ukatili kwa watoto navyo ni sababu kubwa ya kudhalilika kwao.
MWISHO
Wednesday, September 11, 2013
WANAJESHI WAJERUHI RAIA, KAMANDA AKANUSHA
|
||
|
Subscribe to:
Posts (Atom)