Friday, January 30, 2015
NAPE NNAUYE AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUIAMINI CCM MWAKA 2015
NA, STEPHANO MANGO,SONGEA
WANANCHI Wametakiwa Kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi (Ccm) Kuwa Ndicho Chama Pekee Kinachopaswa Kuendelea Kuwaongoza na kutatua Changamoto Zinazowakabili Kuliko Vyama Vingine Vya Siasa Kutokana na Uchanga Wake Pamoja na Sera Zao Kutokukidhi Matakwa ya Wananchi Katika Karne ya sasa
Hayo yalisema Jana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati akiwahutubia Mamia ya Wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Kwenye Mikutano yake Tofauti aliyoifanya Mjini hapa baada ya Maandamano Makubwa yaliyoanza Katika Ofisi ya Ccm Mkoa wa Ruvuma Hadi Kata ya Lizaboni na kufanikiwa kufungua matawi ya chama, miradi mbalimbali ya chama na kuwapatia kadi wanachama wapya
Nnauye Alisema Kuwa Vyama Vingi Vya Siasa Havina dhamira ya Kweli ya Kuwaletea Wananchi Maendeleo bali Vimekuwa vikipiga Kelele ili viwalaghai Wananchi wapate Uongozi ili wajinufaishe wenyewe binafsi na Vyama Vyao
Alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kinatarajia Februari Mosi Mwaka Huu kufanya Sherehe ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwake miaka 38 iliyopita katika Sherehe hizo chama kinajivunia utekelezaji wa ahadi zake na maendeleo makubwa yaliyopatikana kwa kipindi chote cha uwepo wake madarakani.
Alieleza kuwa CCM inaendelea kutekeleza ilani yake vizuri na wataendelea kuisimamia Serikali katika kutimiza ahadi za mwaka 2010 na kwamba maeneo machache yalienda kwa wapinzani kimakosa na kuahidi makosa hayatorudiwa tena katika uchaguzi wa mwaka huu
“ Naomba Niviambie vyama vya Upinzani kuwa kauli mbiu ya Mwaka Huu ya Maadhimisho ya Ccm ni Umoja ni Ushindi, Katiba yetu nchi yetu hivyo chama kimejipanga kuelimisha wananchi namna ya upigaji wa kura katika katiba mpya pia kurudisha maeneo yaliyochukuliwa na vyama vya upinzania katika uchaguzi wa mwaka 2010”.
Alisema kuwa wananchi wana imani kubwa na Ccm hivyo Wapinzani walipanga kwa muda wa miaka mitano na kwamba kodi yao imesha wanapaswa kuondoka kabla hawajafukuzwa na mwenye nyumba kwani havina sera na vimeshindwa kuja na sera mbadala ya kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini
Alifafanua kuwa Mafanikio ya Ccm yametokana na Watendaji wa Serikali kuwa karibu na wananchi kwani kumesaidia kufanikisha maendeleo na kuondoa sintofahamu za wananchi wanaotaka kujua taarifa za maendeleo ya miradi au maeneo husika.
Alisema pia kila mtu kwenye utumishi wa serikali inabidi awajibike katika kufanikisha lengo na asiyeweza inabidi aachie ngazi kwani ni lazima tutangulize utumishi wa umma.
Pia aliwataka vijana kuacha kuingia kwenye makundi ya watu watakaowatumia kisiasa na kabla ya kuwashabiki viongozi fulani kuna umuhimu watafute historia za viongozi hao
MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment