Na Stephano Mango,Songea.
JESHI la polisi mkoaniRuvuma limebaini kuwa mabaki ya mwili wa binadamu yaliyokutwa yamehifadhiwa kwenye mfuko na kutupwa kati kati ya mto Nakawale wilayani Songea hivi karibuni ulikuwa tayari umeshachunwa ngozi na kuchukuliwa mifupa pamoja na kichwa kitendo kilichofanywa na watu wasiojulikana na kisha kutokomea navyo kusikojulikana.
JESHI la polisi mkoani
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 24 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi katika eneo la Nakawale wilayani Songea ambako Afisa mtendaji wa kijiji hicho alipewa taarifa na wananchi kuwa kuna mwili wa binadamu ukiwa umehifadhiwa kwenye kiloba umeonekana upo kati kati ya mto.
Alisema kuwa Afisa mtendaji huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana baada ya kupata taarifa hiyo alikwenda kwenye eneo la tukio ambako aliwakuta wananchi wamekusanyika kisha alifanya mawasiliano na polisi ambao baadaye walifika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na daktari wa serikali kwa ajiri ya uchunguzi.
Aidha alisema kuwa baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa mwili huo ilibainika kuwa mwili huo ulikuwa ni wa marehemu Jafar Shabani mkazi wa kijiji hicho huku ukiwa umechunwa ngozi ,mifupa pamoja na kichwa na kubaki nyama na nguo za marehemu huyo zikiwa kando kando ya mto huo ambazo ndizo zilizopelekea wananchi kugundua kuwa aliyeuawa kuwa ni Shaban.
Kamuhanda ameeleza zaidi kuwa polisi baada ya kufanya uchunguzi zaidi walibaini kuwa siku chache kabla ya tukio hilo marehemu huyo alikuwa amegombana na Said Kandemanje(37) ambaye tayari amekamatwa na anahojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo .
Aidha kamuhanda alisema kuwa uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwepo kwa vitendo vya ufukuaji wa makaburi yaliyoko kwenye vijiji vya nchi jirani ya Msumbiji ambako karibu na mpaka wa Tanzania na kuchukua viungo mbali mbali vya binadamu vinavyodaiwa kupelekwa nchi nyingine kwa uuzaji wa mifupa hiyo ya binadamu.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na matukio hayo ili kuweza kubaini mtandao wa watu wanaofanya vitendo hivyo viovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria kwa hatua zaidi
MWISHO
No comments:
Post a Comment