About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Sunday, August 14, 2011

Moja ya vyoo vinavyolalamikiwa na wanachuo na wakufunzi katika Chuo cha Ualimu Matogoro ambapo kama hatua za makusudi hazitachukuliwa huenda kukaibuka magonjwa ya mlipuko








CHUO CHA UALIMU SONGEA KIPO HATARINI KUPATA MAGONJWA YA MLIPUKO
Na Stephano Mango,Songea
WANACHUO wa chuo cha Ualimu Songea,Wakufunzi na wafanyakazi katika chuo hicho wapo katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali ya mlipuko ukiwemo ugonjwa wa kuhara,kipindupindu na magonjwa mengine ya hewa kutokana na uchafu wa vyoo chuoni hapa
 
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika chuo hicho umebaini kuwa kwa muda mrefu vyoo vya utawala vinaendelea kutumika inngawa vyoo hivyo havijafanyiwa ukarabati kutokana na uchakavu wake na kwamba hata mabomba ya maji katika vyoo hivyo hayafanyika kazi
 
Imebainika kuwa katika vyoo hivyo vya jikoni,dukani,utawala nje,utawala ghorofani vimekuwa chakavu na vimeandikwa kuwa vimefungwa kutoka na ubovu mkubwa lakini kutokana na uhaba wa vyoo chuoni hapo bado vinatumika
 
Uchunguzi uliofanywa katika vyoo vya madarasa ya mwaka wa pili Diploma,bweni la wasichana la Nyerere,mabweni ya Wavulana ya Aggrey,Mandela na Nkuruma vina hali mbaya sana na miuondombinu ya maji imechakaa na kusababisha utandu mkubwa wa uchafu katika sahani za vyoo hivyo
 
Vyoo vingi vimekutwa vikiwa na ndoo ambazo zimekuwa zikitumika kuwekea maji zikiwa tupu na karatasi zimekuwa zikizagaa chooni wakati vyoo hivyo vinapaswa kutumia maji badala ya karatasi
 
Kutokana na uchunguzi huo vyoo vingi chuoni hapo vimekutwa vikiwa vimebandikwa vikaratasi vinavyosomeka kuwa vyoo hivyo vimefungwa lakini kutokana na uhaba wa vyoo vimeendelea kutumika hali ambayo inaweza kuhatarisha afya za watumiaji
 
Uchunguzi umebaini kuwa vyoo hivyo vimekuwa vikisafishwa kwa nadra tena bila sabuni wala madawa maalum ya kusafishia hali inayopelekea kuwa na harufu kubwa kwa watumiaji wa vyoo hivyo na watu wanaoishi pembezoni mwa chuo na kusababisha adha kubwa
 
Juhudi za kumpata Mkuu wa Chuo hicho hazikuzaa matunda kwa madai kuwa uongozi wa Chuo na viongozi wa Chama cha Walimu wa Wilaya Manispaa ya Songea walikuwa wamejifungia ndani kutokana na mgomo wa wakufunzi unaoendelea chuoni hapo
MWISHO


No comments:

Post a Comment