About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Sunday, August 14, 2011

MAHINDI HAYA ENDAPO YATAHIFADHIWA KWA MADAWA MAKALI KAMA VILE KIMATILA HUENDA YAKASABABISHA AFYA ZA WALAJI KUWA MATATANANI KUTOKANA NA SUMU KALI ILIYOPO KWENYE DAWA HIYO,HIVYO NI VEMA MAMLAKA HUSIKA IKACHUKUA HATUA MADHUBUTI KUKOMESHA HALI HIYO




WAKULIMA SONGEA WATUMIA MADAWA MAKALI KUHIFADHIA MAHINDI
Na Stephano Mango,Songea
WAKULIMA wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wamekuwa wakitumia dawa ya aina ya Kimatila ambayo ni hatari kwa afya za binadamu kuhifadhia mahindi katika kipindi hiki cha msimu wa mavuno.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima  kwa kipindi cha mwezi mmoja umebaini kuwa dawa hiyo imekuwa ikitumika kuhifadhia mahindi ambayo wakulima huichanganya na mahindi ili yasiharibiwe na wadudu waharibifu

Tanzania Daima imefanya uchunguzi kwenye Vijiji vya Mpitimbi, Lyangweni, Peramiho, Sinai, Litapwasi na Mpandangindo na kubaini kuwa wakulima wamekuwa wakitumia dawa hiyo inayotumika kwenye zao la kahawa ili lisishambuliwe na wadudu na wao huweka  kwenye mahindi ili yasiliwe na wadudu.

Akizungumza na Tanzania Daima mmoja wa wakulima wanaotumia dawa hiyo kuhifadhia mahindi Pilimina Ngonyani Mkazi wa Kijiji cha Litapwasi anasema amekuwa akitumia dawa hiyo kwa miaka mingi ambapo anasema chupa moja ya dawa hiyo wanayonunua kwa Tsh.2000 wanaichanganya na lita 20 za maji na kuchanganya na mahindi kilo 300.

Mkulima mwingine Alfonce Hyera wa Mpitimbi anasema yeye amekuwa akitumia dawa hiyo kwa kuwa inauzwa bei rahisi na pia inatunza mahindi kwa muda mrefu bila kushambuliwa na wadudu ukilinganisha na dawa yenyewe ya kuhifadhia mahindi iitwayo Super Actellic Powder ambayo huuzwa Tsh.2500 ya unga ambayo huchanganywa na mahindi kilo 300.

Mkulima huyo anafafanua kuwa dawa ya kimatila hutunza mahindi kwa mwaka mmoja bila kushambuliwa na wadudu wakati dawa yenyewe ya kuulia wadudu Super Actellic Powder hutunza mahindi yasishambuliwe na wadudu kwa muda wa miezi sita.

Tanzania Daima iliongea na Boharia wa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Songea Alfred Ndunguru ili kujua kama hifadhi ya chakula wanatumia dawa gani na wananchi wafanyaje ili mazao yao yawe salama na pasitokee madhara ya kiafya kwa binadamu.

Ndunguru alisema wao kama hifadhi wanatumia Dawa ya unga na maji (Actelic ) alisema utumiaji wake kuchanganya mahindi  kisha kupulizia kwa kutumia bomba maalum na vifaa kinga hewa isiwadhuru ambapo wakulima wao wanachanganya mbegu za mahindi kwenye dawa kwa kumwagia mahindi kienyeji kitu ambacho ni hatari kwa afya zao na za walaji.

Alibainisha zaidi kuwa mbegu ya mahindi ikilowanishwa kwenye dawa ina madhara kwasababu dawa itakuwa imepenya kwenye mahindi,hivyo hata mahindi yakikobolewa bado sumu ipo ndani ya punje ya mahindi , alishauri Serikali ione umuhimu kuliona hilo ili kunusuru maisha ya binadamu.

Alisema ni vema Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zake zikatenga bajeti ya kutoa Elimu ya kutunza mazao kwa wakulima, mara baada ya mahindi kukauka yakiwa shambani na kuvunwa tayari kwa kuyahifadhi.

Naye Afisa Ubora msaidizi wa  Mazao wa hifadhi ya Chakula ya Taifa Ruhuwiko Songea Braison Henricki Kiama alisema mazao ya mahindi Mkoani Ruvuma hayana ubora hii ni kutokana na wakulima kuvuna mahindi yao kabla ya kukauka pia wanavuna mahindi na kuto yapepeta.

Alifafanua zaidi kuwa madhara ya kutopepeta kunasababisha mahindi yawe na fangasi wajulikanao kama Afratokisini pia inaweza kusababisha kansa kwa watumiaji wa mahindi kawaida yanatakiwa yawe yamekauka unyevu 13.00 mpaka 13.05 (moisture content).

MWISHO

No comments:

Post a Comment