WANANCHI KUANDAMANA KUSHINIKIZA KUPIMIWA ARDHI, KUNG’OLEWA MKURUGENZI SONGEA
Na Stephano Mango,Songea
WANANCHI wa Kata ya Mshangano, Halmashauri ya Manispaa ya Songea wanatarajia kufanya maandamano makubwa ya amani ya kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwang’oa kazi Mkurungezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Nachoa Zakaria na , Afisa Mipango Miji wake Castory Msigala kwajili yakuwa kikwazo cha maendeleo ya wananchi.
Akisoma tamko la wenyeviti wa serikaili za mitaa wa kata ya Mshangano ambayo imekumbwa na mgogoro mzito wa ardhi, Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mshangano, Paul Mangwe alisema kuwa (kesho) leo wanataria kufqanya maandamano ya amani yatakayo anzia kwenye ofisi ya kata hiyo hadi kwa mkuu wa wilaya ya Songea Thomas ole Sabaya kumfikishia ujumbe wa kutaka kupewa kibali cha kupimiwa ardhi yao na kumuomba Waziri Mkuu kuwang’oa viongozi hao wawili ambao wamekuwa kikwazo kwa zoezi hilo.
“ Sisi wenyeviti wa serikali za mitaa ya Mitendewawa, Namanyigu na Mshangano tulishaomba kibali kwa OCD wa Songea kumjulisha kuhusu maandamano ya amani, kibali tutapata na hata kama hakitapatikana wananchi wamedai lazima waandamane kesho(Leo),” alisema Mangwe.
Alisema ifahamike kuwa wananchi wa kata ya mshangano tangu walipo kutana Agosti 13 mwaka huu walimtaka Mkurugenzi huyo awe amesaini michoro na kibali cha kuiruhusu Kampuni ya Ardhi Plan ltd yenye Makao makuu Dar es Salaam ambayo imekwisha wahi kufanya kazi kama hiyo kwenye Kata ya Mwenge Mshindo mjini hapa iweze kuwapimia wananchi maeneo yao ambayo wamesitisha shughuli ya kuyaendeleza tangu Disemba 2010.
Katika taarifa hiyo Wenyeviti wa Mitaa wa Kata hiyo walisema kwakuwa Mkurugenzi Nachoa na Afisa Mipango Miji wake Msigala wamekaidi matakwa ya wananchi wenye ardhi wa kata ya Mshangano kushindwa kujibu barua ambazo walizipeleka za kutaka kupimiwa ardhi takribani miezi tisa sasa wameshindwa kumuelewa ni kitu gain anachotaka kutoka kwa wakazi wa kata hiyo.
“Tunapata mashaka makubwa na kukosa imani na Viongozi hao wawili(Nachoa na Msigala) kwani pamoja na kutokujibu barua zetu lakini mazingira yamejionyesha kuwa wao wana maslahi binafsi,” walisema wenyeviti hao katika mkutano na waandishi wa habari.
Hata hivyo, walisema wao wapo tayari kufa kuliko kuiachia ardhi ya wapiga kura wao waliowachagua mwaka 2009 katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuwaletea maendeleo.
Walisema kuwa hawaoni mtu mwingine atakaye suluhisha mgogoro huu mkubwa uliodumu kipindi kirefu zaidi ya mtoto wa mkulima Waziri Mkuu Mizengo Pinda mwenye uchungu na watu wanyonge hapa nchini.
Walisema wameshangazwa sana na viongozi wa serikali ya mkoa wa Ruvuma kulifumbia macho swala zito kama hili na hivi sasa wameona wana mtu mmoja tu ambaye wanaamini ana ujasiri wa kumfikishia ujumbe waziri Mkuu na si mwingine bali ni DC wa Songea Thomas Ole Sabaya ambaye hata kama atasema hana mafuta ya kwenda na kurudi Dodoma wao wako tayari kuchanga nauli hiyo ilimradi Waziri Mkuu Pinda apate ujumbe huo wa kutaka kurasmishiwa makazi yao badala ya kujenga kiholela kwenye eneo la Manispaa.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema kibali cha maandamano hayo hakijakamilika kwakuwa hakijakidhi matakwa kama yale ya kuonyesha njia, muda na tarehe ya maandamano.
Kamuhanda amefafanua kuwa tatizo hilo ni kubwa na tayari linatarajiwa kupelekwa kwenye kamati ya ulinzi na Usalama ya mkoa ili kuangalia wapi chanzo cha kuendeleza mgogoro huo hadi watu wafikie hatua ya kutaka kuandamana.
Mwisho
No comments:
Post a Comment