WANANCHI wa Kijiji cha Mkili Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wamemtaka Mkurugezi wa Halmashauri Wilaya ya Mbinga kusimamia zoezi la kupata uongozi wa kijiji hicho kwani kijiji hicho kwa muda mrefu kina uongozi wa mda ambapo shughuli zote huendeshwa na Mtendaji wa kijiji, baada ya aliyekuwa Mwenyeketi wa kijiji hicho John Isdori Tilia kusimamishwa uongozi na Serikali yake yote .
Tuhuma zilizopelekea Mwenyekiti huyo na serikali yake yote kusimamishwa uongozi ni pamoja na kutoitisha mikutano ya serikali ya kijiji kutosoma mapato na matumizi ya kijiji kushindwa kusimamia miradi mbalimbali ya kijiji na wakati mwingine kujishughulisha zaidi na mambo ya starehe na kuacha yale yanayohusu maendeleo ya wanakijiji .
Wanakijiji wa Mkili baadhi yao wametaja miradi ambayo ameshindwa kusimamia ni ujenzi wa kibanio cha mfereji wa maji kwa kilimo cha umwagiliaji ambacho kipo katika mto Ndumbi kijijini hapo ,ujenzi unaendelea wakituo cha afya kwa kujenga nyumba nne za waganga na ukarabati wa barabara itokayo bandari ya Mkili hadi Hospitari ya Litembo .
Wakitoa kero zao kupitia mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ baadhi ya wanakijiji hao walisema toka serikali ya kijiji hicho ichaguliwe hawajasomewa taarifa ya mapato na matumizi ambapo shughuli zote huendeshwa na mwenyekiti aliyesimamishwa uongozi na mtendaji bila wanakijiji kuhusishwa.
Wameongeza kuwa kijiji hicho kina bonde la kutosha kwa fursa ya kilimo cha umwagiliaji wa mpunga ambapo tayari Halmashauri ya Mbinga ilishatoa mradi wa umwagiliaji katika kijiji hicho lakini kwa kukosa uongozi bora wa kijiji,kibanio kilisombwa na maji mara mbili jambo ambalo mkandalasi hakufuatiliwa namna alivyojenga kibanio hicho na ubora wake .
Wamesema kilimo hicho cha umwagiliaji katika bonde lililopo kijijini hapo kingeweza kuwanasua wanakijiji kwa kupata zao la mpunga mara mbili kwa mwaka hivyo wamemwomba mkurugezi wa Wilaya ya Mbinga kuharakisha zoezi la kuwapata viongozi wa serikali ya kijiji ili kuharakisha maendeleo
Walipoulizwa kuhusu tatizo la sumu inayotiwa katika mito inayozunguka kijijini hapo hasa toka eneo milimani walisema vitendo hivyo vya uharibifu vinatendwa na baadhi ya watu kutoka vijiji vya Mahande ,Siasa ,Lundumato,Mkoha,kwa uroho wa kutafuta Samaki ambapo madhara yake huua madhalia yote ya viumbe hai katika mito hiyo ambayo ni Ndumbi ,Mnyamaji,Chipindi,na Luhorochi.
Wanakijiji hao wamempongeza mkurugezi mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Mbinga kwa kuwatia moyo ili wafyatue matofari ya nyumba nne za waganga kwa ajili ya kuimarisha na kupanua kituo cha afya cha Mkili pia kwa ahadi ya kupatiwa gari la kusafirisha wagonjwa siku za usoni toka kituo cha afya Mkili hadi Hospitari za Lihili, Mbinga ,Litembo ,Songea na Peramiho.
Aidha wanakijiji hao wameiomba serikali kuwaimarishia mawasiliano ya simu kwa kuwajengea minara ya Voda,Airtel,Tigo na TTCL,mawasiliano ambayo wanayapata kwa shida kwa kupanda juu ya miti ama kwenye vichuguu.
No comments:
Post a Comment