About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, September 5, 2011

CHADEMA WAMFYATUKIA MGOMBEA UMEYA WA CCM SONGEA CHARLES mHAGAMA

                                Diwani wa kata ya Misufini kupitia Chadema Salum Mfamaji
                                         Katibu wa CHADEMA mkoa wa Ruvuma Dorphini Ghazia
                                         Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime
Na,Stephano Mango,Songea
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimemshukia mgombea wa nafasi ya Umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kupitia Chama cha Mapinduzi(Ccm) Charles Mhagama kwa madai kuwa sio kiongozi makini na muadilifu anayeweza kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa maslahi ya wananchi
 
Akihutubia mamia ya wakazi wa Manispaa ya Songea katika viwanja vya soko la Manzese,kata ya Misufini Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime alisema kuwa nafasi ya Umeya ni nafasi nyeti sana katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea hivyo ina hitaji mtu makini,mwenye hekima,busara na muadilifu wa kuweza kushirikiana na wadau mbalimbali kuweza kulisukuma gurudumu la maendeleo
 
Fuime alisema kuwa kutokana na umuhimu huo mgombea aliyepitishwa na Chama cha Mapinduzi (Ccm)Charles Mhagama ili kuweza kuziba nafasi ya Umeya iliyoachwa wazi na Marehemu Ally Manya aliyefariki mwezi julai 29 mwaka huu,kuwa hana uwezo wa kushika nafasi hiyo kutokana na kujaa tamaa ya kujitajirisha kiharamu kupitia fedha za wananchi
 
Alieleza kuwa Mhagama ni kiongozi mbabe na mwenye kupenda rushwa hali inayodhorotesha maendeleo ya wananchi kwani alishawahi kufanya vitendo viovu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa ushawishi wa rushwa katika ununuzi wa gari ya kuzima moto,uuzwaji wa Katapila la Halmashauri akiwa ni Diwani wa kata ya Matogoro na kiongozi wa Kamati mbalimbali za baraza la madiwani
 
“Mhagama hawezi kuwa kiongozi bora na atakayeweza kutupeleka kwenye ustawi stahiki wa maisha kwani vitendo vyake vingi ni viovu kwani kuna kipindi alikuwa na mahusiano na mwanafunzi mmoja miaka ya nyuma ambapo alikutwa naye kwenye nyumba ya wageni na wazazi wa mwanafunzi huyo na kupelekewa kupigwa viboko hadharani”alieleza Fuime
 
Alifafanua kuwa vitendo hivyo vinadhihirisha ni jinsi gain alivyokuwa mchafu na kiongozi mbovu asiyestahili kupewa majukumu makubwa ya Umeya hasa katika kipindi hiki kilichogubikwa na ufisadi,rushwa na urasimu mkubwa Serikalini
 
Alisema kuwa siku zote Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikiwaacha viongozi wazuri na kuwateua viongozi wabovu ili waweze kukinufaisha chama kwa maslahi yao binafsi hivyo hatuwezi kuongozwa na kiongozi wa aina hiyo na ndio maana tunapaza sauti ili umma ujue na kuwaambia Madiwani wao waliowachagua kutokumpigia kura mgombea huyo wa Ccm kwenye uchaguzi wa Serikali unaotegemewa kufanyika Septemba 25 mwaka huu
 
Alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni mali ya wananchi wote na sio mali ya chama fulani hivyo wananchi pazeni sauti zenu kwa maslahi ya vizazi vilivyopo na vijavyo ili waweze kufaidi rasilimali zilizopo kuliko kuwaachia watu wenye dhamira mbaya wazizoe rasilimali hizo
 
Alieleza kuwa kwa kuwa chama cha Mapinduzi kipo kwa ajili ya kuwanyonya watanzania,kunyanyasa haki za binadamu kwa maslahi ya wachache basi Chadema tutatetea haki za binadamu na kuzuia unyanyasaji wowote na ndio maana tunapaza sauti zetu ili wananchi muamke na kudai maisha yenye ustawi kwani ni haki zenu
 
Awali Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Ruvuma Dorphine Ghazia akingua mkutano huo alisema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi ni Serikali katili sana kwa watu wake ndio maana wanaona wananchi wanahangaika kwa maisha magumu wao wanaendelea kuwakandamiza
 
Ghazia alisema kuwa watanzania hawana huduma bora za afya,miundombinu,elimu,maji wao wanawatukuza wanyama kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kuishi mfano mzuri wa vyura vya kihansi wanalindwa kuliko binadamu,hivyo Chadema kitaendelea kuthamini utu wa binadamu kwa kuwatendea mambo yenye ustaarabu katika maisha yao
MWISHO

No comments:

Post a Comment