About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, September 5, 2011

POLISI RUVUMA INAWASAKA WATU WATANO KWA TUHUMA ZA MAUAJI

                             Na Gideon Mwakanosya, Songea.
 
POLISI mkoani Ruvuma inawasaka watu watano wakazi wa kijiji cha Likuyuseka kilichopo wilayani Namtumbo kwa tuhuma za kumuuwa Issa Lupia (47) wakati wakiwa kwenye kilabu cha pombe  za kienyeji.
 
Akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ ofisini kwake kamanda wa Polisi mkoani hapa Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa moja usiku huko katika eneo la kilabu cha pombe za kienyeji kijiji hapa.
 
Alisema kuwa watuhumiwa hao baada ya kugunduwa kuwa wametenda kosa walitoroka na kutokomea kusikojulikana na kwamba kwa sasa hivi polisi inaendelea kuwasaka watuhumiwa hao ambao wanadaiwa kuwa wametorokea nchi jirani ya msumbiji.

Amefafanua kuwa inadaiwa kuwa kabla ya tukio Lupia aliondoka nyumbani kwake na aliaga kwamba anaenda kwenye kilabu cha pombe za kienyeji kilicho karibu ambako alipofika alimkuta Hamza Saidi ambaye ni rafiki yake akiwa na wenzake wane.
 
Alisema kuwa Lupia aliungana na wenzake walianza kunywa pombe na baadae walianza kutofautiana ndipo ulipotokea ugomvi ambapo Lupia alipigwa ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwilini na kumsababishia kifo papo hapo.
 
Kamanda alisema kuwa watu waliokuwa jirani na eneo hilo walipofika kwenye tukio ghafla watuhumiwa hao walianza kutawanyika mmoja baada ya mwingine na kutokomea kusikojulikana ndipo taarifa ya tukio hilo ilipelekwa kwenye ofisi za serikali ya kijiji na baadae polisi ambao walifika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na mganga wa hospitali ya Mkoa alithibitisha kuwa Lupia amekufa kutokana na kipigo.
 
Alisema kuwa chanzo cha tuki hilo ni ulevi ambao baadae uliwafanya watofautiane na kuanza kumpiga mwenzao Lupia na kumsababishia kifo.
 

No comments:

Post a Comment