Na Mwandishi Wetu,Songea
HALI ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea mjini mkoani Ruvuma ni tete kutokana na madiwani wake saba kutishia kurudisha kadi za chama hicho na kujiuzulu nafasi zao zote ndani ya chama ikiwemo na udiwani kwa kile kilichodaiwa kumpigia kura za hapana mgombea wa unafasi wazi ya umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Wakizungumza na waandishi wa habari jana kwa nyakati tofauti madiwani hao walisema kuwa wao kwa pamoja wameitwa kwenye kamati ya maadili ya chama hicho ili waweze kuhojiwa kwanini waliamua kukisaliti chama na kuungana na madiwani saba wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) na kumpigia kura za hapana mgombea wa nafasi ya umeya aliyepitishwa na Ccm Charles Mhagama katika uchaguzi uliofanyika jana na kuishia na vurugu kubwa kwa kurushiana makonde na matusi ya mwilini
Walisema kuwa ni kweli walimpigia kura za hapana ili uchaguzi uitishwe upya kwa sababu mgombea wa chama chao hatoshi kushika wadhifa huo kwani kuna mambo mengi ambayo ameshindwa kuonyesha uongozi wenye umahili na kwamba Chadema wenye madiwani saba hawakusimamisha mgombea
“Ndani ya chama viongozi walilazimisha na akafanikiwa kupenya kwenye mchakato wa ndani nasi tukasema wamezoea kutuburuza kwa kutulazimisha kupitisha viongozi wanao taka wao kwa maslahi ya wachache sasa awamu hii tunawaonyesha nguvu zetu kwa kumpigia kura za hapana ili wahaibike vizuri mbele za watu wengi”walisema madiwani hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe
Walisema kuwa kumpigia kura za hapana diwani mwenzangu wa Ccm kwenye uchaguzi wowote ule sio dhambi ila kumpigia kura za ndiyo diwani wa Chadema ndio ingekuwa dhambi kwa mujibu wa demokrasia mfu zilizopo ndani ya Ccm sasa tunashangaa kuitwa kwenye kikao cha maadili leo
“Tupo tayari kwa lolote ili wananchi wapime ubabe uliopo ndani ya Ccm kwani wao ndio waliotuchagua hivyo tunapaswa kushirikiana nao katika kulisukuma gurudumu la maendeleo na sio kuwadhurumu rasilimali zao na kuwasababishia ufukara mkubwa miongoni mwao
Juzi ulifanyika uchaguzi wa nafasi wazi ya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo Chadema hawakusimamisha mgombea kwa madai kuwa mchakato mzima wa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki na kwamba Ccm walimsimamisha Diwani wa kata ya Matogoro Charles Mhagama
Katika uchaguzi huo uliotawala na vulugu za kila aina wajumbe waliopiga kura walikuwa 26 hivyo kwa mujibu wa mtangaza matokeo Naibu Meya Mariam Dizumba kuwa Mhagama alipigiwa kura za ndiyo 14 na hapana 12 ndipo madiwani walipoanza kutaka uhesabuji ufanyike upya kwa uwazi kwa maana wanamashaka makubwa na utangazaji wa matokeo ambapo uchaguzi huo haukumalizika
Akizungumza na mtandao huu Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Alfonce Siwale alikiri kuwaita madiwani wote kwenye kikao cha maadili ili waweze kuhojiwa kuhusiana na zoezi zima la uchaguzi wa kuziba nafasi wazi ya umeya na kuongeza kuwa kama madiwani wanataka kujiudhuru nafasi zao itakuwa ni busara kwani mtu mzima alazimishwi jambo
MWISHO
No comments:
Post a Comment