Na Gideon Mwakanosya, Songea
MFANYABIASHA mmoja Habiba Kazembe (45) mkazi wa Mtaa wa Muungano uliopo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma amevamiwa na kundi la watu wanaosaidikiwa kuwa ni majambazi na kuporwa fedha taslimu shilingi milioni 5 akiwa amelala chumbani kwenye nyumba ya kulala wageni ya Mataya iliyopo katika kijiji cha Lusewa Wilayani Namtumbo na wafanya biashara wengine watatu wamejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na majambazi hayo ambayo yalitoroka na kutokomea kusiko julikana.
Walio jeruhiwa kwa kupigwa na risasi wametajwa kuwa ni Edga Kayombo mfanya biashara Mkazi wa Eneo la Lizaboni Manispaa ya Songea, Michael Komba mfanya biashara ambaye ni Mkazi wa Mahenge Songea Mjini na Muhudumu wa nyumba ya kulala wageni wa nyumba ya Mataya Mariamu Azizi .
Habari zilizopatikana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Majeruhi zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea September 15 majira ya saa za usiku huko katika Kijiji cha Lusewa kilichopo Wilayani Namtumbo ambako inadaiwa majambazi ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja wakiwa na silaha aina ya SAR na SMG walivamia nyumba ya kulala wageni kisha waliwajeruhi watu watatu kwa kuwapiga na risasi watu watatu sehemu mbalimbali za miili yao na kumpora mfanyabiashara mmoja shilingi milioni tano nakutokomea nazo.
Mmoja wa majeruhi Edga Kayombo ameuambia mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ jana mchana kuwa yeye amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mkono wa kushoto akiwa amelala kwenye gari ambalo lilikuwa nje ya nyumba ya kulala wageni baada yakukosa vyumba .
Amefafanua kuwa kundi hilo la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivamia nyumba hiyo ya kulala wageni saa 9 usiku yeye akiwa kwenye gari ghafla alisikia mlio wa risasi zikipigwa ndani ya nyumba ya kulala wageni .
Amesema kuwa baada ya kusikia milio ya risasi aliondoka na kwenda ndani ya nyumba ya kulala wageni ambako walikuwa wamelala wafanyabiashara wenzake lakini akiwa anatoka kwenye gari hilo alikutana na watu watatu wakitokea kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni wakiwa na siraha wameshika mikononi ambapo mmoja kati yao alimpiga risasi kwenye mkono wa kushoto.
Ameeleza zaidi kuwa majambazi hao baadaye waliondoka na kutokomea kusikojulikana na yeye alianza kupiga kelele kwa ishara ya kuomba msaada ambapo majirani walifika kwenye eneo la tukio kisha waliwachukua majeruhi hadi kituo cha polisi cha lusewa ambako walipatiwa hati ya matibabu ambako walikimbizwa kwenda hospitali ya serikali ya Mkoa kwa matibabu zaidi.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mkoa Songea Dkt Benedict Ngaiza ameiambia nipashe kuwa majeruhi hao walipokelewa majira ya saa 5 na nusu asubuhi ambapo alibainisha kuwa Kayombo amepigwa risasi kwenye kiganja cha mkono wa kushoto, Komba amepigwa risasi kwenye makalio na Mariam Azizi amepigwa risasi sehemu za siri chini ya kinena na kwamba mpaka sasa risasi moja bado ipo kwenye paja lake wanafanya jitihada ya kuondoa risasi hiyo mwilini.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) George Chiposi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo amedai kuwa limetokea majira ya saa 9 usiku huko katika Kijiji cha Lusewa Wilayani Namtumbo kwenye nyumba ya kulala wageni ya Mataya ambako kundi la Majambazi wakiwa na siraha zinazosadikiwa kuwa ni SAR na SMG waliingia kwenye nyumba ya kulala wageni ya mataya na kupiga risasi na baadaye walifanikiwa kuvamia chumba cha mfanyabiashara mmoja habiba kayombo ambaye alidaiwa kuwa alitokea Tunduru kuja kufanya biashara kwenye mnada na walimpora fedha tasilimu shilingi milioni tano na baadaye walimjeruhi kwa kumpiga makofi na wapangaji wengine walijeruhiwa kwa kupigwa risasi.
Chiposi amesema kuwa watuhumiwa hao baada ya kupora fedha za mfanyabiashara huyo walikimbia na kutokomea kusiko julikana na polisi inaendelea kuwasaka majambazi hao ambao mpaka sasa bado hawajafahamika.
MWISHO
No comments:
Post a Comment