YEBOYEBO YAMGONGA MAMA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO
Na Gideon Mwakanosya,Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linamshikiria mwendesha Pikipiki mmoja Omari Mdoka mkazi wa kijiji cha Mchoteka kilichopo Wilayani Tunduru kwa tuhuma za kumgonga Mwanamke Halima Mohamedi (19) na kusababisha kifo cha mtoto wake aliyekuwa amebebwa mgongoni wakati anatoka shambani.
Akizungumza na Mwandishi wa mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com ,Gideon Mwakanosya jana ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Geoge Chiposi amesema kuwa tukio hilo limetokea September 15 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri katika kijiji cha Mkalola kilichopo Wilayani Tunduru.
SSP Chiposi ameeleza kuwa siku hiyo ya tukio inadaiwa kuwa mwendesha pikipiki Mdoka akiwa anatoka Mchoteka kwenda Kijiji cha Mkalola alimgonga mtembea kwa mguu Halima Mohamedi ambaye alikuwa amembeba mtoto wake mgongoni Asha Mauridi Mwenye umri wa miezi tisa.
Amefafanua zaidi kuwa Mdoka ambaye alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajiri T 813 BLM, aina ya Sunlge alikimbia mara tu ya kutokea ajari hiyo, lakini baadaye wananchi wa kijiji hicho walifanikiwa kumkamata akielekea katika kijiji cha Nalasi.
Hata hivyo Kaimu kamanda wa Polisi SSP Chiposi ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kwamba mwendesha pikipiki alikuwa kwenye mwendo mkali ambao ulisababisha kushindwa kumudu usukani wakati mwanamke huyo Halima Mohamedi akiwa amembeba mwanaye mgongoni akijaribu kumkwepa kandokando ya barabara upande wa kulia ambapo alimgonga na kukimbia na Polisi wanaendelea kufanya upelelezi na utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayo mkabili.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment