Na, Gideon Mwakanosya SongeaMTU mmoja mkazi wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma amekufa papohapo na wengine sita wamejeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Songea mjini kwenda Namtumbo kuacha njia na kupinduka.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Naftari Mantamba amesema kuwa tukio hilo limetokea oktoba 24 mwaka huu majira ya saa 8.00 mchana katika eneo la Mletele Songea mjini.
Mantamba amemtaja aliyefariki dunia kuwa ni Sabina Similia(80) mkazi wa eneo la Faraha Store Mbinga mjini na kwamba waliojeruhiwa amewataja kuwa ni Failuna Komba(70) na Hassan Ally(40) wote wakazi wa kijiji cha Mgombasi kilichopo katika wilaya ya Namtumbo.
Amewataja majeruhi wengine kuwa ni Flora Mamzi(39) mkazi wa mtaa wa Furaha Store Mbinga mjini,Amina Komba(63) mkazi wa kata ya Lizabon Songea mjini,Mohammed Hassan(50) mkazi wa mtaa wa Ruhila Songea mjini na Omary Mtumbuka(42) mkazi wa kijiji cha Litola kilichopo wilayani Namtumbo.
Kaimu Kamanda Mantamba amefafanua kuwa basi hilo lenye namba za usajili T761 ATN aina ya Isuzu Forward ambalo lilikuwa limebeba abiria kutoka Songea mjini kuelekea Namtumbo na kwamba lilikuwa likiendeshwa na Hamis Chidumule(35) mkazi wa kata ya Ruvuma Songea mjini likiwa kwenye mwendo mkali liliacha njia na kupinduka.
Amesema kuwa majeruhiwa mpaka wamelazwa katikahospitali ya mkoa kwenye wodi za majeruhi ambapo hali zao zinaendelea vizuri na kwamba chanzo cha ajali hiyo gari hiyo ilikuwa kwenye mwendo mkali hali iliyosababisha dereva ashindwe kumudu ukukani na hivyo kuacha njia na kupinduka.
Hata hivyo polisi mkoani hapa imefanikiwa kumkamata dereva wa gari hilo na kwamba kwa sasa uchunguzi unaendelea kufanyika ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment