Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yasiyo kuwa ya Serikali yanayojishughulisha na masuala ya Ukimwi Mkoani Ruvuma (RUNOWA) Mathew Ngarimanayo akiwasalimia wananchi waliohudhuria Mahafari ya Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sabasaba Simon Lupanga akisalimia ndugu,jamaa,walezi na wazazi waliofika katika Mahafari hayo kuwapongeza wahitimu wa shule hiyo
Mwenyekiti wa Shule hiyo Joseph Kalande akitoa nasaha zake kwa wahitimu wa shule ya Msingi Sabasaba,kulia ni Mratibu wa Elimu Kata ya Matarawe Theofrida Mango,wa kwanza kushoto Mwalimu Mkuu wa Sabasaba Simon Lupanga,wa pili Mwenyekiti wa RUNOWA)Mathew Ngarimanayo
Mgeni Rasmi katika Mahafari ya Shule ya Msingi Sabasaba Mwenyekiti wa RUNOWA Mathew Ngarimanayo akiwahutubia wananchi waliohudhulia Mahafari hayo
Wazazi na Walezi wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Mgeni Rasmi Mathew Ngarimanayo aliyoitoa katika Mahafari hayo |
Na Stephano Mango,Songea
SERIKALI imetakiwa kusimamia kikamilifu mpango wa mifuko ya jamii ya kusimamia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kusaidiwa na jamii wanamoishi kwa kutumia kamati maalumu ya kuratibu watoto hao kuanzia ngazi ya mitaa hadi Wilaya ili kuweza kuleta ustawi na maendeleo ya watoto hao
Wito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayojishughulisha na masuala ya Ukimwi Mkoani Ruvuma(Runowa) Mathew Ngarimanayo wakati akihutubia kwenye mahafari ya darasa la saba Shule ya Msingi Sabasaba
Ngarimanayo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafari hayo alisema kuwa suala la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ni bomu kubwa ambalo linazinyemelea familia zetu na taifa kwa ujumla hivyo kila mwananchi anatakiwa aamke na kutambua kuwa watoto hao wanaongezeka siku hadi siku katika jamii zetu
Alisema kuwa kila mdau popote alipo aliangalie suala hilo na achukue hatua stahiki ya kupunguza wimbi hilo kwanikwasasa takwimu za watoto hao mkoani Ruvuma imefika jumla ya watoto 32,532 ambapo sababu zinazosababisha hali hiyo ni pamoja na mimba za utotoni,kuzaa nje ya ndoa,umasikini wa kipato katika familia,mifarakano ya wanandoa,magonjwa mbalimbali,ajali za barabarani na maafa mengine
Alisema kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mwaka 2006 na 2008 ilifanya zoezi la utambuzi wa watoto hao katika Wilaya za Mkoa wa Ruvuma na wakaweka utaratibu ambao wananchi walipaswa kuchukua na kuhakikisha watoto hao wanasaidiwa katika jamii wanamoishi
Alieleza zaidi kuwa katika ngazi za mitaa,Kata,Wilaya viliwekwa vyombo ambavyo vinaweza kukaa na kujadili kwa kina masuala ya watoto hao na kuweka mikakati ya kumaliza tatizo hilo kwa kutumia Kamati za Ukimwi kuanzia ngazi ya mitaa hadi Wilaya kwani Kamati hizo zingekuwa zinafanya kazi yake kikamilifu tatizo la watoto hao lingekwisha
“Wahitimu tambueni elimu mliyoipata ni ya msingi tu na kwamba safari mliyonayo ni ndefu maishani ili mfikie mafanikio ya kweli,msibweteke naomba Mungu awajalie wote mfaulu kwenda Sekondari,vyuo na kuendelea pia mkawe mfano wa tabia njema huko nyumbani kwa kuwa nyie ndio mnaotegemewa kushika nafasi mbalimbali katika jamii,epukeni vitendo viovu ambavyo vinaweza kufuta ndoto zenu katika maisha”alisema Ngarimanayo
Awali akisoma risala ya wahitimu hao Sauna Juma alisema shule hiyo ina watoto waishio katika mazingira hatarishi 17 ambapo kati yao wa 4 wanahitimu leo na kwamba shule ina kabiliwa na changamoto mbalimbali za ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu
Akijibu risala hiyo mgeni rasmi Ngarimanayo alichangia mifuko 10 ya saruji na kuliagiza shirika la Swaat/Sedeco ambalo linafanya kazi katika Kata ya Matarawe ambapo shule ya Sabasaba ipo kuwatambua watoto ngo hao na kuwaingiza katika mpango ili waweze kuhudumiwa haraka iwezekanavyo kadiri ya mahitaji ya vipaumbele vya watoto wenyewe
MWISHO
No comments:
Post a Comment