About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Sunday, October 23, 2011

WATUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA KWA KOSA LA MAUAJI NA MWINGINE AACHIWA HURU

Na Augustino Chindiye, Tunduru

MAHAKAMA kuu Kanda ya Songea imewahukumu kifungo cha miaka mitatu kila mmoja mtu na dada yake baada ya kukiri na kupatikana na hatia ya kufanya kosa dogo la kuua bila kukusudia na kumuachilia huru mtoto wa miaka 14.

Akitoa hukumu hiyo Jaji wa Kanda ya Songea Jaji Hamisa kalombola alisema kuwa adhabu hizo zimetolewa baada ya kuzingatia hoja zilizotolewa na upande wa Jamhuri uliokuwa ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali Hamimu Nkoleye aliyeiomba Mahakama hiyo iwahukumu kifungo cha maisha huku upande wa utetezi ulioongozwa na Wakili wa kujitegemea Sebastian Waryuba akiiomba Mahakama hiyo iwapatie adhabu ndogo wateja wake akidai kuwa kukubali kwao kumeipunguzia usumbufu Mahakama hiyo.

Kaka na dada waliohukumiwa kutumikia kifungo hicho cha miaka mitatu Jela ni Hashim Msusa Ibrahim na Mwanahawa Msusa Ibrahim waliokuwa wanakabiliwa na Shauli la mauaji namba 8/2011 la kumuua marehemu Halifa abdalah February 2/2010 wakiwa wanagombea mfuko tupu wa kubebea mahindi wa kiroba cha mbolea ambapo tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Lijombo Wilayani Tunduru.

Shauli jingine lililotolewa maamuzi na kufikia maamuzi ya kumuachilia huru yaani (Anconditional Discharge) baada ya Mahakama hiyo kumtia hatiani kwa kosa dogo la kuua bila kukusudia ni Shauli Namba 2/2011 lililo kuwa likimkabili Mwamini Mwandope (14) aliye muua marehemu Salome Sanga baada ya kutokea ugomvi kati yao katika tukio lilitokea katika Kijiji cha Hanga Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.

Jaji Hamisa kalombola aliendelea kueleza kuwa mahakama yake   imeamua kutoa adhabu hizo kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 119 kifungu kidogo (2a) na kifungu kidogo cha (4) vya sheria ya kanuni ya adhabu vinavyoipatia mamlaka Mahakama hiyo.
  
Awali kabla ya kutolewa kwa adhabu hizo watuhumiwa hao walitiwa hatiani na mahakama hiyo baada ya kukiri kufanya kosa dogo la kuua bila kukusudia  baadaya kusomewa kosa la kumuua bila kukusudia ambapo Mtoto aliye achiliwa huru alidaiwa kumuua marehemu Salome Sanga kwa kumchoma kisu baada ya kutokea ugomvi kati yao huku wanandugu Hashimu na Mwanahawa wakidaiwa kumuua kwa kumpiga na mangongo kichwani marehemu Halifa Abdala katika ugomvi wa kugombea mfuko tupu.

Jaji Kalombola alisema kuwa pamoja na mambo mengine Mahakama yake imeridhishwa na hoja zilizotolewa na Wakili wa Upande wa utetezi Sebastian Waryuba kwamba pamoja na mambo mengine kikiwemo kigezo cha kukubali kosa hilo mbele ya Jaji na kuiondolea Mahakama usumbufu mteja wake anastahili kupatiwa adhabu yenye unafuu chini ya kifungu cha 119 cha Sheria ya watoto namba 21ya mwaka 2009.

Awali katika ujenzi wa hoja za Utetezi kwa mteja huyo wakili msomi wa kujitegemea Sebastian  Waryuba alidai kuwa chini ya makosa hayo wateja wake wanapaswa kunufaika chini ya kifungu cha 119 cha sheria za kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyia mapitio mwaka 2002 ambapo wakati mtuhumiwa akitenda kosa hilo Agosti 28/2010 na huku akimwelezea Mtoto Mwamini Mwandope kuwa wakifanya kosa hilo alikuwa na umri wa miaka 13, na sasa  ana Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 6 ambaye alijifungua wakati akiwa mahabusu.

Alisema kipitia kifungu hicho mteja wake anastahili kupewa adhabu ya kifungo cha nje ama kutumikia adhabu ya kutumikia jamii huku Mwanasheria wa Serikali Hamimu Nkoleye akiiomba mahakama hiyo impatie adhabu ya kifungo cha maisha.
Mwisho

No comments:

Post a Comment