About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, November 7, 2011

KARDINARI PENGO AWAPONGEZA WATANZANIA KWA KUITUNZA AMANI NA MSHIKAMANO WA TAIFA MIAKA 50 YA UHURU

 Na Augustino Chindiye,Tunduru
IMEELEZWA kuwa wakati Taifa la Tanzania likielekea kutimiza Miaka 50 ya UHURU  Wananchi wake wameishi katika amani na utulivu licha ya kuishi katika lindi la umasikini uliopindukia hali inayo onesha kuwa mgao wa rasilimali za nchi hauendi kwa usawa.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Baraza la umoja wa Maaskofu Africa Mwasisi wa Jimbo la Tunduru-Masasi, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardnali Pengo wakati akiongea katika maadhimisho ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Jimbo la TUNDURU –Masasi mjini hapa.

Alisema mbali na kuishi katika machungu hayo Watanzania wanatakiwa kupongezwa kutokana na kuishi katika Umoja licha ya kuwepo kwa tofauti za udini na akawataka waumini wa Madhehebu ya Kikristo kuyatumia maadhimisho ya Jubilei hiyo kugeuza mienendo na kuanza maisha mapya ya kiroho na kuondoa kasoro za kijamii kwa vile uhuru umo pia katia Uchumi, Siasa na jamii.

Kardinali Pengo ambaye alikuwa mgeni katika maadhimisho hayo aliongeza kwa kukemea kejeli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya watu kuwa uenezaji wa Injili ambao umekuwa ukifanywa na makanisa si chochote wakati  bila juhudi hizo huenda nchi ingekwisha vurugika na kuivunja amani hiyo.

Akiongea na waamini katika ibada ya Misa takatifu iliyofanyika katika kanisa kuu la Mtakatifu Xafery, Askofu wa Jimbo la TUNDURU-Masasi Mhashamu Castory Msemwa alisema maadhimisho ya Uhuru wa nchi yetu iwe changamoto ya kuwafanya viongozi waliopewa mamlaka kutambua nafasi zao na kurudisha haki za jamii hasa waliopo vijijini ambao ndio walipa kodi hodari lakini wakiwa hawaoni manufaa yatokanayo na kodi zao.

Alisema maadhimisho hayo yalifanye Taifa lifungue milango ya kutoa na kupeana haki na stahili za kila mtu ili kuyafikia maisha Bora na si Bora maisha kwani Uhuru wa kweli ni ule unaomfanya mtu awe katika kupata mambo yote ya msingi katika maisha yake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na uongozi wa Jimbo hilo, jimbo la TUNDURU- Masasi lilianzishwa oktoba 17/1986 chini ya Mhashamu Askofu Polycarp Pengo.

No comments:

Post a Comment