Na, Augustino Chndiye Tunduru
JUMUIYA ya watu wa Korea (KOICA) imeahidi kutoa msaada wenye jumla ya Walimu sita (6) ili wasaidie kufundisha Masomo ya sayansi katika Shule Tano kati ya Shule 20 za Sekondari zilizopo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Jumuiya hiyo Hwng Jin Hee katika hafla fupi ya kukabidhi Mwalimu Mmoja kati ya walimu hao iliyofanyika katika ofisi za Afisa Elimu wa Shule za Sekondari wa Wilayani humo kwa maelekezo kuwa Mwalimu huyo Lee Hyoo Kyung ataanza mara moja kufundisha katika Shule ya Tunduru Sekondari.
Jin Hee alisema kuwa KOICA imepokea kilio cha ukosefu wa walimu wa masomo ya Sayansi kwa vitendo ambapo kwa kuanzia wamemleta mwl. Hyoo Kyung na baada ya muda mfupi ujao watawaleta walimu wengine wanne ambao wamepangwa kufundisha katika shule za Sekondari Mataka, Masonya,FrenkWeston, Nandembo na Mbesa zilizopo wilayani humo.
Alisema nia ya nchi yake ni kusaidia Tanzani Walimu wengi zaidi wa Masomo ya Sayansi ambao wameonekana kuwa na upungufu mkubwa hapa nchini na kwamba hadi sasa KOREA imekwisha leta jumla ya Walimu 100 kupitia Shirika hilo na wanaendelea kutoa huduma hiyo katika maeneo mbalimbali ya Tanzani.
Akizungumzia msaada huo Afisa elimu Shule za Sekondari wa Wilaya ya Tunduru Alli Mtamila alisema kuwa msaada huo umefika kwa wakati na kwamba idara yake inaamini kuwa Walimu hao watawasaidia wanafunzi wa Shule hizo kuwainua kitaaluma.
Mwl. Mtamila aliendelea kueleza kuwa wakati hayo yakiendelea takwimu zinaonesha kuwa idara yake inakabiliwa na upungufu wa walimu 158 kati ya walimu 289 wanaohitajika kufundisha katika Shule hizo huku takwimu hizo zikionesha kuwa walimu waliopo ni 164 tu.
No comments:
Post a Comment