Nahodha wa Timu ya NBC Emmanuel Ntobi akizungumza na waandishi wa habari
Na Stephano Mango,Songea
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) tawi la Songea wametamba kuwanyeshea mvua ya magori watani wao wa jadi Benki CRDB katika mechi ya kirafiki inayotarajiwa kuchezwa Novemba 20 mwaka huu katika uwanja wa Majimaji
Akizungumza na Waandishi wa habari jana kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majiamaji Songea Nahodha wa timu ya NBC Songea Emmanuel Ntobi alisema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwani wachezaji wote wana ari nzuri wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo ya aina yake
Ntobi alisema kuwa lengo mechi hiyo ni kukuza urafiki,ujirani na undugu kati ya taasisi za kifedha na wateja wao kiujumla kwani muda mwingi wamekuwa wakikutana katika shuguli za kibenki tu na kufanya wateja wasifurahi pamoja na wafanyakazi wa taasisi za kibenki
Alisema kuwa lengo jingine ni kujenga afya njema za wafanyakazi wa taasisi hizo za kifedha kwani michezo licha ya kuwaweka watu pamoja pia ni nguzo muhimu ya kujenga afya stahiki kwa binadamu yoyote
Alisema kuwa siku hiyo ni muhimu sana kwa kutengeneza na kudumisha mtandao baina ya wateja na maafisa wa taasisi hizo za benki na kwamba kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazoporomoshwa na maafisa wa benki hizo muhimu kibiashara nchini
Alifafanua kuwa mechi hiyo ya kirafiki ni hatua muhimu ya kuendelea na mipango stahiki ya kuboresha shughuli za kibenki na wateja wa taasisi za kifedha ndani ya mkoa na nje ya mkoa ili waweze kufaidi huduma za taasisi hizo kikamilifu na kukuza mahusiano
Nahodha huyo Ntobi alisema kuwa baada ya mechi hiyo kukamilika kutakuwa na programu nyingine mbalimbali za ujrlani mwema ikiwa pamoja na midaharo kuhusu thamani ya shilingi ya Tanzania na kudorora kwa uchumi wake
Alieleza zaidi kuwa katika mechi hiyo ya aina yake mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Meneja wa Kampuni ya Tigo Mkoa wa Ruvuma Wilfred Nestory na kwamba wateja wa taasisi za fedha na wapenzi wa soka wanapaswa kuhudhuria mechi hiyo muhimu
MWISHO
No comments:
Post a Comment