About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, December 7, 2011

MJADALA WA MAPUNGUFU YA MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA,2011 WAENDELEA SONGEA

Mheshimiwa Regia Mtema(MB) akisindikizwa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime kuingia kwenye Ukumbi wa Parokia ya Bombambili kwa ajili kutoa semina ya mapungufu ya Muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba,2011
Wanachama wa Chadema Mkoani Ruvuma wakicheza wimbo wa Chadema Peoples Power ikiwa ni ishara ya kuwapongeza Wabunge wa Chama hicho walivyotoka Bungeni mara baada ya Tundu Lssu(MB) kuwasilisha maoni ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba,2011

Katibu wa Chadema Jimbo la Kawe Powel Mfinanga akisoma kwa umakini Muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba,2011

Katibu wa Chadema Jimbo la Kawe Powel Mfinanga akifafanua jambo,kutoka kulia ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Dolphin Ghazia,Mwenyekiti wa Chadema mkoa Joseph Fuime,Mbunge wa Viti maalum Chadema Regia Mtema, kushoto ni Mwenyeki wa Chadema Wilaya ya Songea Peter Mboya 
Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Regia Mtema akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime wakati wanachama wa chama hicho wakitoa maoni yao mbalimbali kuhusu Muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba,2011

No comments:

Post a Comment