About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, December 9, 2011

ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE NA KUMTUNDIKA KWENYE MTI AKIDAI AMEJINYONGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Mwandishi Wetu,Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linamsaka Omary Almasi Mkazi wa Kijiji cha Pacha nne kilichopo katika Kata ya Nakapanya Wilayani Tunduru kwa tuhuma za kumuua mke wake wakiwa shambani kisha kumtundika juu ya mti akisingizia kuwa mkewe amejinyonga.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael kamuhanda zimesema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 1 mwaka huu majira ya saa 8.10 mchana huko katika Kijiji cha Pacha nne.
Kamuhanda amemtaja mwanamke aliyeuawa na mume wake kuwa ni Somoe Mastawi (48) Mkazi wa Kijiji cha Pacha nne Wilayani Tunduru.
Amefafanua kuwa inadaiwa siku hiyo kabla ya tukio hilo kutokea Omary na mke wake Somoe waliondoka nyumbani kwao na kuelekea shambani kulima shamba la Mahindi na baadae majira ya saa nane na dakika kumi katika hali ambayo siyo ya kawaida Somoe alianza kupata kipigo kutoka kwa mume wake na kumsababishia kifo.
Amesema kuwa mwanamke huyo Somoe aliuwawa na mume wake wakiwa Shambani na baada ya kumfanyia kitendo hicho cha kinyama mke wake alichukua kamba na kumfunga shingoni kisha alimtundika juu ya mti mrefu kwa kusingizia kuwa mwanamke huyo amejinyonga.
Kamanda Kamuhanda ameeleza zaidi kuwa Omary baada ya kugundua kuwa watu wameshafahamu kuwa kitendo hicho cha kinyama amekifanya alikimbia na kutokomea kusikojulikana na kwamba Polisi bado wanachunguza chanzo cha tukio hilo huku wakiendelea kumsaka mtuhumiwa.
 TUKIO LINGINE………………………………….
Na Mwandishi Wetu,Songea

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDONDOKEWA NA KIFUSI KWEMYE SHIMO ALILOKUWA AMELALA
SELEMANI Yahaya  (30) Mkazi wa Mtaa wa Mkuzo Kata ya Mshangano katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma amekutwa akiwa amekufa kwenye shimo alikokuwa akilala kila siku baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga wakati mvua zikiendelea kunyesha.
Akizungumza na Mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com jana Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa za usiku huko katika Mtaa wa Mkuzo uliopo Kata ya  Mshangano.
Amefafanua kuwa siku hiyo ya tukio Said Yassin Mkazi wa eneo la Mtaa wa Mshangano akiwa anapita akitokea Mjini kuelekea nyumbani kwake aligundua kuwa kwenye shimo alilokuwa akilala Yahaya limefukiwa na kifusi kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Alisema kuwa Yassin baadaye alikwenda kwa majirani na kuwajulisha kuwa shimo ambalo alikuwa akilitumia Yahaya  kwa kulala limebomolewa na mvua na wananchi walipofika kwenye eneo hilo waligundua kuwa Yahaya amefukiwa na kifusi .
Alieleza zaidi kuwa Uongozi wa Serikali ya Mtaa kwa kushirikiana na Wananchi wa eneo hilo walifanya jitihada za kutoa taarifa Polisi na baadaye walianza kazi ya kufukua shimo hilo na kumkuta Yahaya akiwa tayari amekwisha kufa.
Kamanda Kamuhanda amesema kuwa inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo marehemu wakati wa uhai wake alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa akili ambao ndio ulimsababishia kulala kwenye shimo hilo.
TUKIO LINGINE…………………………….
Na Mwandishi Wetu, Songea
MWANAMKE AFA BAADA YA KUPIGWA NA RADI AKITOKEA SHAMBANI KWAKE 
AMINA Mstafa (45) Mkazi wa Matarawe katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma amekufa papo hapo baada ya kupigwa na radi wakati akiwa njiani anatoka shambani huku akiwa amevaa shingoni simu yake ya mkononi iliyokuwa imefungwa kwa kamba.
Akizungumza na www.stephanomango.blogspot.com jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 8 mchana huko katika Kijiji cha Mrogoro kilichopo eneo la Peramiho Wilaya ya Songea Vijijini.
Kamuhanda amesema kuwa Amina kabla ya kukutwa na mauti alikuwa anatoka shambani kwake kulima shamba la  mahindi na alipofika njiani mvua zilizokuwa zimeambatana na radi zilianza kunyesha.
Ameeleza zaidi kuwa Amina akiwa anaendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwa mguu huku akiwa amevaa shingoni simu yake ya mkononi iliyokuwa imefungwa kwa kamba ghafla radi ilimpiga na kumsababishia kifo papo hapo.
Amefafanua kuwa baada ya radi kumpiga Amina na kumsababishia kifo watu waliokuwa njiani walikwenda eneo la tukio kisha walitoa taarifa kwa Serikali ya Kijiji na baadaye Polisi ambao walifika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na Mganga ambaye alithibitisha kuwa Amina tayari alishakufa muda mrefu kwa kupigwa na radi.
 MWISHO

No comments:

Post a Comment