Na Steven Augustino, Tunduru
SERIKALI imewataka Viongozi wa Dini waliopewa mamlaka ya kubariki Ndoa kuachana na tabia za kufungisha ndoa kwa waumini wao ambao wataenda kuomba kupatiwa huduma hiyo huku wakiwa hawajapima virusi vya Ukimwi,
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha wakati akiongea na wananchi waliojitokeza katika Maadhimisho ya siku ya Kutafakari mikakati ya kupambana na janga la Ukimwi yaliyofanyika Kiwilaya Katika Kijiji cha Makande kilichopo katika Tarafa ya Lukumbule Wilayani humo.
Pamoja na agizo hilo pia Madaha aliwataka Wazazi na Walezi kuto
ziachia Televisheni na Mitandao ya Kompyuta iwalelee Watoto wao bali wao wenyewe watimize wajibu wao katika utoaji wa malezi yenye maadaili yanayo endana na maudhui ya ki Africa na kuwaepusha watoto wao kupata Mimba za utotoni na Virusi vya Ukimwi .
Akifafanua hotuba hiyo Madaha alisema kuwa endapo Mashekhe na
Mapadre watasimamia kwa vitendo wataisaidia jamii kujenga tabia za kupima afya zao kwa hiari ili kujitambua na kupanga mikakati ya maisha bila kuwa na mashaka.
Sambamba na maagizo hayo Dc, Madaha pia alitumia nafasi hiyo kutoa elimu ya Ukimwi kwa kuwataka Makungwi na Manyakanga kuachana na tabia za kutoa masomo yasiyo endana na maadili zikiwa ni juhudi za mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Aliseam hivi sasa makungwi na manyakanga hao wamekuwa wakitoa elimu inayowapatia udadasi hasa watoto wa kike na kuwataka kwenda kujaribisha kwa vitendo hali ambayo imekuwa iki wasababishia madhara makubwa yakiwemo ya kupata Mimba na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Akizungumzia msimamo wa Serikali juu ya mapambano hayo Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Jalia Msangi alisema kuwa ingawa msimamo wake hauendani na maadili ya Dini aliwahimiza
wananchi kuvaa na kutumia kinga mbadala iliyoidhinishwa na wataalamu wa Afya ili kujikinga na maambuikizi mapya ya VVU na Ukimwi.
Alisema katika kukabiliana na Janga hilo Halmashauri yake imekuwa ikiongeza juhudi za kughalamia utoaji wa elimu Sekondari kwa Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 461 pamoja na kutoa huduma kwa Wajane na Wagane 20 kuanzia mwaka 2009.
Awali akisoma Risala ya maadhimisho hayo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru Dkt. Alex Kazula, Mganga kutoka kitengo cha Ushauri nasaha Dkt. Modestus Ponera alisema kuwa baada ya Serikali kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za Upimaji wa VVU na UKIMWI watu wengi zaidi wamekuwa wakijitokeza ili kupatiwa huduma hiyo.
Dkt. Ponera aliendelea kueleza kuwa pamoja na kuwepo kwa juhudi hizo idara yake imekuwa ikikabiriwa na changamoto kubwa ya jamii kutobadilitabia za kuachana na ngono zisizo salama, na akaongeza kuwa baada ya idara yake kutoa elimu ya kuachana na Unyanyapaa idadi ya Wagonjwa ambao huenda kupatiwa huduma ya tiba na matunzo imeongezeka kutoka wateja 52 mwaka 2005 hadi wateja 2935 mwaka huu.
Nje ya Ukumbi wa maadhimisho hayo nikakutana na kundi la vijana wa uhamasishaji wa kupima afya kwa hiari la Jipange Pambana na Ukimwi(JIPAU) ambapo Mratibu wa kundi hilo Mchungaji Simoni Magonga akaeleza kuwa hivi sasa Shirika lake limefanikiwa kufungua matawi katika vijiji vyote vya Wilaya hiyo zikiwa ni juhudi za kuisaidia Serikali katika mapambano hayo
No comments:
Post a Comment