MBUNGE wa Jimbo la Tunduru Kusini Alhaji Mtutura Abdalah Mtutura amedai kuwa hakubaliani na hataunga mkono tamko la Uongozi wa Serikali ya Wilaya hiyo juu ya zoezi la kupiga marufuku wa magari ya mizigo aina ya CANTER kuchukua abiria.
Alhaji Mtutura alitoa kauli hiyo alipotakiwa kutoa maoni yake juu ya Oparesheni ya kamatakamata ya magari hayo inayotekelezwa na Jeshi la Polisi Wilayani humo wakidai kuwa magari hayo hayaruhusiwi kubeba abiria na mizigo.
Akifafanua taarifa hiyo Mbunge huyo alisema kuwa msako huo unaendeshwa kwa uonevu mkubwa kwa madai kuwa miundombinu ya Barabara na mazingira ya Wilaya hiyo bado hayaruhusu kuwepo kwa mabasi ya abiria yatakayo weza kufanya safari katika maeneo ya Vijiji vyote,
Adhi Mtutura aliishauri Serikali kuweka mikakati ya utoaji wa elimu ya kuwataka madereva wa magari hayo aina ya CANTER kubeba abiria kidogo pamoja na kuwashauri wamiliki wake kuyasajiri ili yapatiwe leseni ya kubeba abiria pamoja na kulipa kodi ili waendelee kutoa huduma kwa wananchi.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Wilaya hiyo Mkoani Ruvuma waliiomba Serikali kuingilia kati tatizo hilo la kukosekana kwa Usafiri wa kuelekea vijijini na kuhakisha kuwa huduma hiyo inapatikana muda wote ili waweze kuondokana na kero ya upatikanaji wa huduma wakidai kuwa hivi sasa wanapata wakati mgumu wanapotaka kwenda kufuata mahitaji yao.
Miongoni mwa waliopaza sauti zao juu ya malalamiko hayo ni pamoja na Mwenyejiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tunduru Kanduru kasim Kanduru, Alli Selemani na Halima Saidi ni miongoni Wananchi ambao walipaza sauti zao baada ya kukosa usafiri kwa siku mbili baada ya Jeshi la Polisi Wilayani humo kuanzisha msako kabambe wa kukamata na kuyaondo kabisa magari ya mizigo ambayo yamekuwa yakibeba abiria hao kutoa Tunduru Mjini kuelekea Vijijini.
Wakati wananchi hao wakipaza sauti zao nao wamiliki wa magari hayo wamelilalamikia Jeshi hilo kwa kitendo hicho cha uonevu unaolenga kudidimiza utendaji wao kibiashara na kuwakwamisha kulipa mikopo waliyo nunulia magari hayo.
Wakiongea kwa masharti ya kuomba majina yao yasitajwe kwenye mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com kwa hofu ya kushughulikiwa wafanya biashara hao walisema kuwa mbali na uonevu wanaofanyiwa na Jeshi hilo wa kutozwa faini isiyo pungua Tsh. 150,000 pindi wanapo kamatwa pia mpango huo unalenga manufaa ya wajanja wachache kutafuta Fedha za sikuku za mwisho wa mwaka.
Walisema kama zoezi hilo lingekuwa ni halali lilitakiwa kufanyika nchi nzima ama ndani ya Mkoa mzima lakini cha kushangazo zoezi hilo limefanyika Wilayani Tunduru pekee hali inayo onesha ulakini katika uhalali wake
Akiongea kwa njia ya Simu ya kiganjani Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha mbali na kukiri kuwa magari hayo yamezuiliwa kuendele kutoa huduma hiyo ,wananchi walisema hatua hiyo ni sawa na kukatika kwa mawasiliano kati ya wananchi wa Tunduru Mjini na vijijini hasa kwa wasio kuwa na uwezo wa kukodi Pikipiki ambaapo hatima yao haijulikani walidai kuwa zoezi hilo ni agizo la Serikali na linatakiwa kutekelezwa nchi nzima.
``Ni kweli zoezi hilo lipo na linaendelea, lakni hebu fanya mawasiliano na Kamanda wa Polisi wa Wilaya kwa ufafanuzi zaidi`` alisema Dc, Madaha na kuongeza kuwa yeye alipatiwa taarifa hizo na Kamanda huyo kuwa agizo hilo linatekelezwa baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wake Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda katika maelezo yake alikiri kuwa zoezi hilo ni halali na kwamba tayari wamiriki wa magari hayo walikwisha pewa maelekezo ya kufanya mabadiliko kwa kununua mabasi ili waendelee kutoa huduma hiyo miezi mitatu iliyo pita lakini walikaidi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment