Diwani Mstaafu na Mdau wa Michezo Golden Sanga(Sanga One) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ligi ambayo inatarajia kuanza hivi karibuni mjini hapa
Na Stephano Mango,Songea
CHAMA cha mpira wa miguu katika Manispaa ya Songea(SUFA) kimezitaka vilabu kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Sanga One Cup ambayo yamepangwa kufanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Sokoine katika Manispaa hiyo.
Akizungumza mjini hapa jana, Katibu msaidizi wa SUFA, Godfrey Mvula alisema kuwa mashindano hayo yatahusisha vilabu vyote ndani ya Manispaa hiyo ambavyo vina usajili wa kudumu kutoka kwa msajili wa vyama vya michezo nchini na vile visivyokuwa na usajili huo.
Mvula alisema mashindano hayo yatadhaminiwa na mmoja wa wadau wa soka na pia Mwenyekiti wa SUFA katika Manispaa hiyo, Golden Sanga maarufu kwa jina la Sanga One yenye lengo la kusaka vipaji vipya na kuviibua ili kuwafanya wachezaji hao kuwa tegemeo na hazina kwa Manispaa mkoa na Taifa kwa ujumla.
Alisema mashindano hayo yatakuwa chachu na mbinu ambayo itasaidia SUFA kuwapata wachezaji wenye vipaji na wanaojituma wawapo uwanjani badala ya kuwatafuta kwa kuwateua kupitia kwenye mashindano ya ligi ya wilaya au mkoa na kuishia kutafuta maslahi yao binafsi badala ya mpira uliomweka hapo.
Alieleza kuwa bingwa wa mashindano hayo ataondoka na kitita cha fedha taslimu Sh. 200,000/=, wa pili atazawadiwa fedha Sh. 100,000/= na mshindi wa tatu ataambulia fedha Sh.70,000/=, mchezaji bora atazawadiwa fedha taaslim Sh.20,000/= na timu itakayoonyesha nidhamu ya ndani na nje ya uwanja watapata fedha Sh.20,000/=.
Alisema gharama ya uchukuaji wa fomu imepangwa kulipia Sh.10,000/= ambayo itapenda kushiriki mashindano hayo na zitarejeshwa fomu hizo Januari 26 mwaka huu saa 10:30 jioni kwenye ofisi za SUFA alidai mchezaji atakaye bainika amesajiliwa na timu zaidi ya moja jina lake litaondolewa kushiriki mashindano hayo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment