Na Stephano Mango,Songea
WANACHAMA wa Chama Cha ushirika cha Akiba na Mikopo cha walimu Songea Manispaaa wameshauriwa kuacha tabia ya kujitoa uanachama kutokana na kukosa uvumilivu baada ya mikopo yao kuchelewa kutolewa kwa wakati au wanapokosa mikopo na badala yake wametakiwa kuwa wavumilivu.
Wito huo umetolewa jana na Meneja mikopo wa benki ya NMB tawi la Songea Derick Fidelis wakati akifungua mkutano mkuu wa 14 wa wanachama wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Songea Club.
Amesema,Wanachama wanapaswa kuwa wavumilivu na si kukimbilia kujitoa pindi mikopo waliyoomba kutoipata kwa wakati na badala yake wajue kuwa matatizo hayo ni ya kawaida hivyo wasikate tamaa wala kukimbia matatizo.
“Walimu tunapaswa kuwa wavumilivu tuache tabia ya kujitoa uanachama pindi tunapokosa mikopo au kucheleweshewa mikopo , tuwe wavumilivu matatizo ni jambo la kawaida ,nyinyi ni wadau wa kubwa wa NMB ili benki iendelee tunawategemea sana kwani mapato mengi ambayo yanaingia benki yanatokana na michango ya walimu,na mikopo mingi tunawakopesha walimu,”alisema Derick.
Aidha, Meneja mikopo ameahidi kuwa benki hiyo itaendelea kuboresha huduma zaidi ili kufanikisha malengo ambayo wateja wao wakiwemo walimu wanahitaji , ameishauri bodi ya chama hicho kukaa na kuomba mkopo ili kuweza kumalizia jengo lao ili kuinua uchumi wa chama hicho.
Akitoa salamu wakati wa mkutano huo Mwenyekiti wa chama hicho Martin Challe amewataka wanachama hao kuendelea kuwa wajasili na kutokubali kuyumbishwa au kushawishiwa kujitoa uanachama na watu ambao wasiopenda na ustawi na maendeleo ya chama hicho.
“Tayari kunawachama ambao wamejitoa ukiuliza wanadai kuwa kwa sababu uchumi wa chama siyo mzuri na kuchelewa kupata mikopo waliporudi kuomba tena uanachama nasi tumewakataa kwani walikimbia baada ya kuona tumeyumba,”alisema.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment