Timu hizo kabla hazijaanza mashindano zikisalimiana
Mechi kati ya Police Fc na Shujaa Fc ikiendelea ambapo mpaka mpira unamalizika Police Fc 1 na Shujaa Fc 0
Baadhi ya mashabiki wakiangalia mechi kati ya Police Fc na Shujaa Fc
Na Stephano Mango, Nyasa
MASHINDANO ya mpira wa miguu yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Wilaya mpya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma Kapteni John Komba na kushirikisha timu 10 kutoka kata ya Lituhi yamefunguliwa rasmi
Akifungua mashindano hayo mwandaaji wa Mashindano hayo Mbunge Kapteni John Komba alisema kuwa mchezo wa soka unapendwa na watu wengi na unapochezwa huleta furaha kwa wachezaji na mashabiki
Komba alisema kuwa mara nyingi vijana wa kata ya Lituhi walikuwa wanaomba nianzishe mashindano ya soka ili waweze kufurahi na kukuza vipaji vyao
“Nilikubali maombi yao na kuanzisha mashindano haya yanayoshirikisha timu 10 kutoka ndani ya kata ambayo nimeyazindua ili vijana wapate burudani, wajenge afya zao na kubadilishana mawazo namna ya kuwa vijana wenye mawazo chanya ya kujenga nchi yao”alisema Komba
Alieleza kuwa vijana hao kwa kuhitaji mashindano hayo kumeonyesha kuwa hawapendi kupoteza muda wa kuzurula, kutenda vitendo viovu hasa muda wa jioni baada ya kutoka katika shughuli za kilimo au ujasiliamali
Alisema kuwa msindi wa kwanza katika mashindano hayo atapata zawadi ya kombe na fedha shiingi 150,000, msindi wa pili shilingi 100,000 msindi wa tatu 50,000 ambapo timu zilizobaki ambazo zimeshiriki zitapata zawadi ya shilingi 20,000 kila timu
Alifafanua kuwa ili mashindano hayo yawe ya kisasa zaidi nimetengeneza nguzo za magoli (miamba) nimetoa jezi 3 za waamuzi kwa maana ya muamuzi wa ndani na wawili wa pembeni, pia nimetoa jezi 10 kwa timu zilizoshiriki zote na kwamba gharama zake kwa jumla ni shilingi milioni 3
Awali Mratibu wa mashindano hayo Mosi Zamtanga alisema kuwa kabla ya mshindano hayo timu shiriki zilipitia michakato mbalimbali ambapo kwa zile ambazo zilikidhi vigezo vilivyoweka ndizo zilizo sajiliwa kushiriki mashindano
Zamtanga alizitaja timu zinazoshiriki mashindano hayo kuwa ni Nkaya Boys, Lituhi Sekondari, Mzalendo, Shujaa, Dodoma, Ngingama, Njomole, Majeshi, Police na Astone Villa
Mwisho
No comments:
Post a Comment